Wamiliki wa mabasi waonywa juu ya kupandisha ovyo nauli za mabasi hasa mwishoni mwa mwaka.

Wamiliki wa mabasi waonywa juu ya kupandisha ovyo nauli za mabasi hasa mwishoni mwa mwaka.
picha ikiwaonyesha abiria wakisubiri usafiri katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo.

Dar es salaam.
Imeelezwa kuwa Kila kipindi cha mwisho wa mwaka, hasa mwezi wa Desemba, Watanzania wengi wanasafiri kurudi nyumbani kwao kwa ajili ya kuungana na jamaa zao kusherehekea sikukuu za Krismass na mapumziko ya mwisho wa mwaka. Utamaduni huu unakua kwa kasi na unachangia kusukuma maendeleo ya vijiji wanakotoka.
Kutokana na wingi wa abiria hao, kila mwaka mahitaji ya usafiri kwa kipindi hicho yanazidi kuwa makubwa kuliko huduma ya usafiri uliopo. Kutokana na hali hiyo, baadhi ya watoa huduma ambao sio waaminifu huchukulia kipindi hicho kama njia ya kuvuna zaidi kutoka kwa watumiaji kinyume na masharti ya leseni zao. Aidha, kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri, baadhi ya abiria hukubali wenyewe kulipa zaidi kusudi wapate kusafiri.




Kutokana na hali hiyo, Baraza  la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na Majini limewataka wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani kupitia umoja wao (TABOA) kufuata masharti ya leseni zao na kutoza nauli zilizoidhinishwa na SUMATRA. Aidha, Baraza linatoa wito kwa wamiliki wote wa Mabasi kuwahimiza wafanyakazi wao wanaokata tiketi katika vituo mbali mbali nchini kuwa waaminifu kwa waajiri wao na wateja wao.

Akizungumza na wanahabari jiini Dar es salaam mapema hii leo katibu mendaji wa baraza hilo Dkt. Oscar Kikoyo ametoa wito kwa watu wote wanaotarajia kusafiri kipindi cha mwisho wa mwaka kufanya maandalizi ya safari zao mapema ikiwa ni pamoja na kufanya booking na/au kukata tiketi zao mapema ili kuepukana na matatizo ya kulanguliwa tiketi..
"nawashauri abiria wote kutonunua tiketi za safari zao kutoka kwa wapiga debe au vishoka katika eneo la kituo cha mabasi cha Ubungo au vituo vingine nchini kote"alisema Dkt KIKOYO


Aidha Baraza hilo limetoa wito kwa TABOA na watumishi wao kuzingatia kanuni usafirishaji (Transport Licensing (Public Service Vehicles) 2017 (GN No. 421) hususani kanuni 25 (b) (iii) na Kanuni 38 (1) (b) ili kuepuka adhabu wanazoweza kupata kutokana na kukiuka kanui hizo sambamba na kuhakikisha madereva wao wanaendesha magari kwa mwendo unaokubalika ili kuepukana na ajali za barabarani.
Hata hivyo baraza hilo limetoa wito wake kwa mamlaka mbali mbali kama zinazohusika na masuala ya usafiri ulivyoainishwa hapa chini
  1. Magari yanayopewa vibali vya muda yafanyiwe ukaguzi  wa kina kabla ya kukata tiketi.
  2. Watoa huduma wachache hasa wale wanaopewa vibali vya muda waache mara moja kufanya udanganyifu katika nauli.
  3. Vibali vya muda mfupi ni kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kuna usafiri wa kutosha kipindi hiki cha Krismass na mwisho wa mwaka
  4. Abiria wote wawe makini kwenye ukataji wa tiketi, hakikisha tiketi uliyopewa ina kumbukumbu zako sahihi na nauli sahihi uliyolipa
  5. Kituo cha ubungo kina vijana wanaobeba mizigo, kwanza kubalianeni bei kabla hajabeba mzigo wako, pili hakikisha kijana anayebeba mizigo yako amekupatia kadi yake yenye namba iliyoandikwa kwenye koti lake, nyuma na mbele na kwenye troli lake


Comments