SHULE YA BETHELI MISSION YAWATAKA WAZAZI KUWEKEZA KWENYE ELIMU KWA WATOTO WAO.

 SHULE YA BETHELI MISSION YAWATAKA WAZAZI KUWEKEZA KWENYE ELIMU KWA  WATOTO
 


DAR ES SALAAM.
 Wazazi nchini wametakiwa kuifanya elimu kama kipaumbele chao kwa watoto ili kuwajengea watoto hao misingi bora ya maisha 

Hayo yamezungumzwa  jijini Dar es salaam na  meneja msaidizi shule ya msingi Bethel Mission Alvins Nyapala wakati akizungumza na chombo hiki juu ya mipango na mikakati ya shule ya betheli Mission katika kukuza elimu hapa nhini.

Hata hivyo mwalimu Alvins ameongeza kuwa kuna haja kubwa kwa wazazi kuelewa kuwa elimu ndiyo kitu pekeekitakachowaokoa watoto wao kama kitazingatiwa ipasavyo kwa wazazi kujitoa kwa hali na mali katika kuhakikisha wanapata elimu bora.

"wazazi wengi wanapuuzia sana elimu na wanavipa kipaumbele vitu ambavyo siyo lakini elimu wanaacha nyuma hivyo sisis kama Bethel Mission tumekuwa tukiwasisistiza wazazi kuwekeza katika elimu za watoto wao kwani nchi nyingi zilizoendelea duniani ziliwekeza katika elimu hivyo ndo maana nasi tumewekeza katika elimu"alisema Alvins.


Kuhusu shule ya Bethel  Mission Bw Alvins amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo ya mitihani mbali mbali ikiwemo ya darasa la saba jambo lililowapa nguvu wao kama shule na hatimaye kuanzisha kampasi nyingine ya shule hiyo katika eneo la Mbezi,Msakuzi ili kuendelea kutoa elimu bora kwa watoto wa kitanznia na hatimaye kujenga taifa bora.

Aidha ameongeza kuwa kutokana na changamoto ya wazazi kutokulipa ada kwa wakati shule hiyo iliamua kuweka mihula minane ya ulipaji ada ili kuwarahisishia wazazi katika suala la ulipaji wa ada hivyo kujenga mazingira rafiki kati yake na wazazi wa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo na kuongeza kuwa pia wamekuwa wakitoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wazazi,wanafunzi na hata wakaazi wa maeneo hayo ili kuwajengea uwezo wa kujiajiri.


"Shule yetu ni ya Missioni ipo chini ya Kanisa la Wasabato wa Matengenezo, inaendesha Nursary na Primary na ni ya mda mrefu sana, kwa ukweli shule hii imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma na tunaamini mafanikio haya yamechangiwa pia na jamii inayotuzunguka hivyo tumekuwa na program ya kutoa elimu hiyo ya ujasirimali kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu.

Shule ya Betheli Mission ni shule binafsi inayopatikana katika eneo la makuburi,Ubungo jijini Dar es salaam na pia ina kampasi katika eneo la Mbezi,Msakuzi

Comments