NEC YAONGEZA SIKU UANDIKISHAJI WAPIGA KURA DAR,WANANCHI WAFUNGUKA

NEC YAONGEZA SIKU UANDIKISHAJI WAPIGA KURA DAR,WANANCHI WAFUNGUKA
 Dar es salaam
Kufuatia muitikio mkubwa wa wananchi kujitokeza katika kujiandisha katika daftari la kudumu la wapiga kura tyme ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeongeza muda wa siku 3 wa uandikishaji katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa ya Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Uchanguzi wa Tume hiyo Dkt Wilson Charles amesema kuwa kusogezwa kwa zoezi hilo kumetokana na maombi mbalimbali katika vituo vya uandikishaji ambapo pia wananchi walitaka wapewe muda zaidi wa kujiandikisha.

Dkt.Charles amesema baada ya maombi hayo walifanya kikao cha Februari 19 kwa ajili ya kutathmini zoezi hilo na kuamua kuongeza muda wa kujiandikisha. Amesema vituo vyote vitafunguliwa kama kawaida kuanzia saa mbili hadi saa 12 jioni.
Hata hivyo tovuti hii ilitembelea maeneo mbali mbali mbali ya jiji hilo ambapo wakazi wa mtaa wa Luhanga kata ya kisukuru wilayani Ilala wameipongeza hatua hiyo ya tume kuongeza muda wa uandikishaji ili kuwafanya wananchi wengi zaidi wajiandikishe na kupata haki yao ya muhimu kikatiba ya kupiga kura katika uchaguzi wa mkuu wa madiwani,wabunge na rais ambao unatarajia kufanyika baadaye mwaka huu.
   ''tunaipongeza sana tume ya uchaguzi kwa hatua hii kwani tunaona hata hapa kituoni leo tulikuwa watu wengi bado hatujajiandikisha kwa hiyo kwa hatua hii sasa tutapata fursa ya kujiandikisha na kupiga kura hivyo niwaombe watu wote hasa vijana wenzangu tujiandikishe kwa wingi''alisema Evance Shao mkaazi wa kata ya kisukuru jijini Dar es salaam.
 Muda uliongezwa katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura ni siku tatu ambapo zoezi hilo litaitimishwa Februari 23, 2020.



TOVUTI YA HABARI101TANZANIA INATOA RAI KWA WATANZANIA WOTE KUJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA ILI KILA MWANANCHI APATE FURSA YA KUSHIRIKI KATIKA KUCHAGUA VIONGOZI WATAKAOLILETEA TAIFA MAENDELEO.

Comments