ZITTO ACHAGULIWA TENA ACT,MAALIM SEIF NAYE AULA







Dar es salaam
Na

Chama  Cha ACT WAZALENDO kimefanya kimekutana jijini Dar es salaam katika mkutano wake mkuu wa Taifa wenye lengo la kujadili mafanikio ya chama hicho tangu kuanzishwa kwake sambamba na kufanyika uchaguzi wa viongozi wakuu wa chama.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo kiongozi mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe emesema kuwa chama hicho ndiyo chama pekee kilicholenga uzalendo na umoja kwa watanzania bila kujali itikadi zao.


Hata hivyo  Wajumbe wa Mkutano huo Mkuu Taifa wamemchagua tena Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, zittokabwe kuwa Kiongozi mkuu wa chama baada ya kupata kura 276 sawa na 73.6% huku mpinzani wake IsmailJussa akiambulia kura 91 sawa na 24.2%. Hata hivyo, kura 8 zimeharibika.

Naye aliyekuwa mshauri wa chama hicho Maalim Seif Sharif amemshinda mpinzani wake Yeremia Maganja katika kinyanganyiro cha nafasi ya mwenyekiti wa chama na Sasa ndiye mwenyekiti wa  chama hicho Taifa.


Comments