FMJ HARDWARE YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KUTOFUNGA BIASHARA,YATANGAZA MNADA MKUBWA WA VIFAA VYA UJENZI NCHINI




FMJ HARDWARE YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KUTOFUNGA BIASHARA,YATANGAZA    MNADA MKUBWA WA VIFAA VYA UJENZI  NCHINI


Meneja Mauzo wa Kampuni ya Vifaa vya Ujenzi ya FMJ, Frederick Sanga, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mnada wa vifaa vya ujenzi utakaofanyika Mei 30 mwaka huu katika ofisi za FMJ Buguruni Kisiwani jijini Dar es Salaam.




DAR ES SALAAM.
Kufuatia kauli aliyoitoa siku chache zilizopita rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli  kuwa Tanzania haitofunga biashara yoyote katika kipindi hichi cha mlipuko wa virusi vya COVID19  vinavyosababisha homa kali ya mapafu     Corona ,Kampuni  ya usambazaji na uuzaji wa vifaa vya ujenzi ya FMJ  HARDWARE LIMITED  imesema inaungana mkono hatua hiyo ya serikali ambayo imetoa mwanga kwa biashara mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza jijini Dar es salaam, meneja mauzo wa kampuni hiyo Fredrick   Sanga amesema wao kama kampuni ya usambazaji na uuzaji wa vifaa vya ujenzi wanamshukuru Rais Magufuli kwa hatua hiyo kwa kuendelea kutengeneza wepesi kwa wafanyabiashara kufanya biashara zao huku wakiendelea kuchukua hatua mbali mbali katika kujikinga na Corona.

’Ndugu waandishi sisi kama FMJ tunaipongeza hatua ya serikali yetu inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli kwa kutengeneza wepesi na kutofunga biashara hali ambayo imechangia biashara mbalimbali kuendelea kufanyika nchini hakika hili ni jambo jema’’alisema Bw Sanga

Aidha katika hatua nyingine kampuni hiyoiliyopo Buguruni kisiwani  jijini Dar es salaam  imetangaza kufanya mnada mkubwa wa uuzaji wa vifaa mbalimbali vya ujenzi ambao haukuwahi kufanyika hapa nchini hivyo kwa mara ya kwanza kampuni hiyo itauza bidhaa zake za ujenzi kupitia mnada huo utakaofanyika kwa njia ya mtandao na kutangazwa mubashara ‘LIVE’ na vyombo mbali mbali vya habari vya mtandaoni hapa nchini.


Meneja mauzo huyo alisema bidhaa zitakazouzwa ni pamoja na bati, nondo, rangi, bomba na vifaa vyote ambavyo vinahusika na ujenzi kwa kuzingatia ubora uliothibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Mnada huo unafanyika ikiwa ni hatua ya kuunga jitihada za serikali ya awamu ya tano ya kujikinga na maambukizi ya Corona  sambamba na kuwapunguzia mzigo mkubwa wananchi wakati  wakitafuta sehemu sahihi ya manunuzi ya bidhaa za ujenzi vyenye kiwango na ubora ule ule kwa gharama nafuu katika wakati huu wa mapambano dhidi ya janga la Corona.

 ’FMJ Hardware iliona kuja na promosheni hiyo kupitia mnada kwa njia ya mitandao itasaidia sana hata katika kupambana na Corona na kama kutakuwa na mwitikio mkubwa  katika mnada huo utakaowahusisha wakaazi wa jiji la Dar es salaam kwa kuanzia na tutaangalia namna ya kuufanya kuwa endelevu na kuwafikia wateja wengi nchini kote hivyo tunawaomba wananchi kushiriki    kwa manunuzi ya bidhaa bora kwa gharana nafuu  ’’alisema Bw  Sanga





Mnada  huo mkubwa utakaohusisha bidhaa mbalimbali za ujenzi unatarajiwa kufanyika jumamosi ya May 30,2020 kuanzia saa saba mchana kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ikiwemo TanzaniteTV,AyoTV,GlobalTV ,Dar mpyaTV  Onliune na Icon TV

Hata hivyo kwa wananchi ambao wangependa kushiriki kwa   kununua bidhaa katika mnada huo wanaweza kuwasiliana na FMJ Kwa namba 0652  312438 ,0716902995  au 0717478770


meneja mauzo wa kampuni ya vifaa vya ujenzi ya  FMJ HARDWARE LTD ,Fredrick Sanga akionyesha moja ya bidhaa zitakazouzwa katika mnada huo.




moja ya bidhaa za kunawia mikono hasa kipindi hiki cha janga la Corona vinavyouzwa na kusambazwa ka kampuni ya FMJ Hardware .

Comments