FMJ HARDWARE YAZINDUA PROGRAME UUZAJI WA VIFAA VYA UJENZI,MTANDAONI
FMJ HARDWARE YAZINDUA PROGRAME UUZAJI WA VIFAA VYA UJENZI,MTANDAONI
Na mwandishi wetu.
Dar es salaam
Kampuni ya usambazaji na uuzaji wa vifaa vya ujenzi [FMJ]ya
jijini Dar es salaam leo imezindua programe yake ya uuzaji wa vifaa vya ujenzi
kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ili kuwawezesha wananchi kupata huduma
hiyo kwa haraka na kwa wakati zaidi.
Akizungumza na wanahabari katika hafla ya uzinduzi huo
meneja mauzo wa kampuni hiyo Fredrick Sanga amesema kuwa njia hiyo itarahisisha upatikanaji
rahisi wa vifaa vya ujenzi kwa wakaazi wa jiji la Dar es salaam ambapo mteja
atakayeagiza vifaa vingi zaidi atapelekewa vifaa vyake popote alipo ndani ya
jiji hilo bila malipo ya ziada.
‘’ndugu wanahabari
tumekuja na progrme hii mpya na kwa sasa wateja wetu watapata punguzo kubwa la
bidhaa zetu na kwa ufanisi zaidi na katika kipindi cha mwanzoni mwa usambaaji
wa virusi vya corona wateja wengi walikuwa hawanunui bidhaa ila tangu rais Dkt
John Magufuli alipotoa tamko kuwa watanzania waendelee kuchapa kazi hatimaye
wateja wameendelea kuagiza vifaa vya ujenzi kwa wingi hivyo sisi kama FMJ
tunamshukuru sana rais Magufuli kwa utendaji wake’’ alisema Bw Sanga.
Aidha ameongeza kuwa kwa sasa wameanza kufanya mnada kupitia
vyombo mbali mbali vya habari ambao umerushwa mubashara na vyombo hivyo na mwitiko umekuwa mkubwa sana huku
akiongeza kuwa watanzania kwa sasa wamehamasika kununua vifaa vya ujenzi
vinavyotengenezwa na viwanda vya ndani jambo ambalo limechagizwa na
uimarishwaji wa viwanda vya ndani chini ya usimamizi wa wizara ya viwanda na
biashara.
Hata hivyo
ameongeza kuwa wao kama wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi wataendelea kuiunga
mkono serikali ya awamu ya tano kupitia jemedari wake Rais Dkt John Magufuli katika
uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha wanauza kwa wingi bidhaa zinazozalishwa na
viwanda vya hapa nchini.
Kampuni hiyo
ya uuzaji na usambazaji wa vifaa vya ujenzi [FMJ]ambayo iko katika eneo la
buguruni kisiwani katika manispaa ya ilala jijini Dar es salaam imekuwa kampuni
ya kwanza kuuza bidhaa zake za ujenzi kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya
habari mubashara ‘LIVE’ na imeahidi kuendeleza programe hiyo na hatimaye
kuifikia nchi nzima.
Hata hivyo kwa wananchi ambao wangependa kushiriki kwa kununua bidhaa katika mnada huo wanaweza kuwasiliana na FMJ Kwa namba 0652 312438 ,0716902995 au 0717478770
Comments