SHIRIKA LA ADRA LATOA MSAADA WA VIFAA KINGA HOSPITALI YA TEMEKE,KITUO CHA AFYA TEMEKE SDA.
SHIRIKA LA ADRA LATOA MSAADA WA VIFAA KINGA HOSPITALI YA TEMEKE,KITUO CHA AFYA TEMEKE SDA.
Dar es salaam
Shirika la maendeleo na maafa nchini
Tanzania lililo chini ya kanisa la waadventista wasabato [ADRA]limetoa msaada wa vifaa kinga kwa hospitali ya rufaa ya mkoa
Temeke pamoja na zahanati pamoja na kituo cha afya cha kanisa la waadventista
wasabato Temeke SDA vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 8 kwa lengo la
kuwezesha mapambano dhidi ya virusi vya Covid19 vinavyosababisha ugonjwa wa homa kali ya mapafu Corona.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya
vifaa hivyo yaliyofanyika jijini Dar es salaam,Askofu wa kanisa la waadventista
wasabato jimbo la kusini mwa Tanzania Mark
Malekana alisema kuwa vifaahivyo ambavyo ni pamoja na vitakasa
mikono,barakoa na mavazi maalum ya kujikinga na virusi vya Corona kwa wahudumu wa afya [PPE’s]ni
mwendelezo wa shirika la ADRA katika kusaidia sekta ya afya hapa nchini
sambamba na kuiunga mkono serikali katika mapambano juu ya Corona.
‘’tumetoa hapa leo vifaa hivi vikasaidie mapambano dhidi ya Corona ikiwa
ni mwendelezo wa shirika la ADRA ambalo lilianzishwa mwaka 1973 kwa lengo la
kusaidia shughuli mbali mbali katika jamii ikiwemo maji,afya na elimu hivyo
tutaendelea pia katika hospitali nyingine na hatutoi msaada kwa kuangalia misingi
ya kidini,kikabila au itikadi nyingine yoyote bali tunatoa kwa manufaa ya
watanzania wote na pia tunamshukuru Rais Magufuli kwa kuruhusu shughuli nchini
kuendelea kama kawaida kwa kuzingatia tahadhari za afya’’alisema Askofu
Malekana.
Aidha Askofu Malikana amevitaka vyuo
vikuu,vyuo vya elimu ya kati na shule za sekondari nchini ambazo zinatarajiwa kufunguliwa tena june mosi
mwaka huu kupanga ratiba zao za masomo kwa kuzingatia umuhimu wa ibada na Imani
za watu hivyo wasiweke ratiba zinazoingilia mpaka siku za kusali na badala yake
watoe fursa za kufanya ibada kwa wanafunzi katika siku za ibada kwani hata
kupungua kwa maambukizi ya virusi vya corona kumesababishwa na maombi ya
Watanzania hivyo shule na vyuo viheshimu ratiba ya siku za ibada.
Kwa upande wake mwakilishi wa mganga
mkuu wilaya ya Temeke Dkt Grace Mtangu
ambaye alipokea msaada wa vifaa kinga hivyo amelishukuru shirika la ADRA na
kanisa la waadventistawasabato nchini kwa kujitoa katika katika sekta ya afya
kwa kutoa misaada katika hospitali za serikali sambamba na kuendelea kutoa
huduma za afya katika vituo vya afya vya kanisa hilo ambavyo vinaisaidia serikali na jamii husika katika sekta ya afya huku akiyataka mashirika
mengine ya dini kuendelea kuiga mfano huo mzuri wa shirika la ADRA TANZANIA.
‘’hakika sisi kama hospitali ya rufaa ya mkoa,Temeke tumefurahishwa na
jinsi shirika la ADRA na kanisa la waadventista wasabato lilivyojitolea kwa
kutoa vifaa kinga hivi ambavyo vitaisaidia hospitali katika mapambano dhidi ya
magonjwa mbalimbali ikiwemo Corona hivyo pia nawaomba wakaazi wa Temeke na watanzania
kwa ujumla tendelee kuchukuatahadhari juu ya ugonjwa wa corona kwa kufuata
miongozo inayotolewa na wizarayetu ya afya’’alisema Dkt Mtangu.
Naye mkurugenzi wa huduma za afya wa
kanisa la waadventista wasabato jimbo la kusini,Dkt Watson Mwabase amelishukuru shirika la ADRA Kwa msaada wa vifaa
kinga hivyo vilivyotolewa pia katika kituo cha afya cha kanisa cha Temeke SDA
kwa kusema kuwa vitasaidia watumishi wa kituo hicho katika mapambano dhidi ya
ugonjwa wa Corona.
Comments