TLP KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI KATIKA UCHAGUZI MKUU,YAUNDA KAMATI MAALUM KUMFANYIA KAMPENI
TLP
KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI KATIKA UCHAGUZI MKUU,YAUNDA KAMATI MAALUM KUMFANYIA KAMPENI
DAR ES
SALAAM
Chama cha Tanzania
Labour Party [TLP] kimesema hakitaweka
mgombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye
mwaka huu na badala yake kitamuunga mkono rais Dkt John Magufuli kama mgombea
pekee wa urais katika uchaguzi huo.
Akizungumza
na wajumbe wa mkutano mkuu uliokutana hii leo jijini Dar es salaam,mwenyekiti
wa chama hicho Dkt Augustino Mrema amesema kuwa chama hicho kimefikia maamuzi
hayo kwa kauli moja ya kumuunga mkono Rais Magufuli kutokana na utendaji kazi
wake katika kulipigania taifa la Tanzania na kuchochea kasi ya maendeleo.
Hata hivyo
Dkt Mrema amesema kuwa chama hicho
kimeshuhudia maendeleo makubwa hasa katika suala la elimu bure,ujenzi wa
miundombinu ya barabara na madaraja ,kuboreshwa kwa bandari ,kufufua shirika la
ndege ,kuinua sekta ya afya pamoja na kupambana na suala la ufisadi hivyo
wameona hakuna anayestahili kuendelea kuwa katika nafasi hiyo isipokuwa ni Dkt
John Magufuli.
‘’tumeridhika
sana sisi kama TLP ,tumeangalia ilani yetu ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 yote
ambayo tuliahidi kwa wananchi yametekelezwa na Rais Dkt John Magufuli ‘’alisema
Mrema.
Naye katibu
wa itikadi na uenezi wa chama cha
mapinduzi [CCM]Humphray Polepole ameipongeza hatua ya chama hicho kumteua Rais
Magufuli na kumuunga mkono kama mgombea wa urais kwa mwaka 2020/2025 huku akivitaka vyama vingine vya siasa kuiga
mwenendo wa chama cha TLP kwa kuachana na siasa za uchochezi ambazo zinataka kuligawa Taifa kwa kutumika
na mabeberu wasiolitakia amani taifa letu.
Kwa upande
wake naibu msajili wa vyama vya siasa hapa
nchini Sisty Nyahoza amesema chama cha TLP hakijavunja katiba kumfanya
Rais Magufuli kama mgombea urais na kumuunga mkono kwa asilimia 100 na kuitaja
hatua ya chama hicho kama maendeleo makubwa katika mabadiliko ya kisiasa hapa
nchini.
Aidha katika
hatua nyingine chama hicho kimeunda kamati maalum ya kumfanyia kampeni Rais Magufuli bega kwa bega kote nchini na
kamati hiyo itatumika katika kunadi sera zake
na miradi yote ya maendeleo aliyoitekeleza
Comments