CUF Yatagaza kurejesha Ngome Yake Pemba Wachama Wake Waibwaga ACT
CUF Yatagaza kurejesha Ngome Yake Pemba Wachama Wake Waibwaga ACT
Chama cha wananchi CUF kimewataka wanachama wake kutojihusisha na mpango wowote wa kukihujumu Chama hicho kwani atakaebainika kuhusika atachukuliwa hatua kali na chama hakitamhurumia yeyote.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na mahusiano na umma wa chama hicho Mhandisi Mohamed Ngulangwa ambapo amesema wanachama na viongozi waaminifu wasikubali kutumiwa na yeyote kuhujumu chama.
Hayo yamejiri katika ziara ya siku 4 ya Mwenyekiti wa Chama hicho Prof Ibrahim Lipumba na kummomonyoa Kwa nguvu Maliim Seif kutengeneza taharuki na mgogoro wa Chama hicho na kupora baadhi ya Mali zake kutumiwa na Chama cha ACT wazalendo ikiwemo majengo.
Aidha amesema kupitia ziara hiyo wamepokea wanachama zaidi ya 700 kutoka Act Wazalendo ambao wamesema wanajutia uamuzi wao wa kukihama chama hicho bila kufikiri kwa kina ila baada ya kuelezwa ukweli kuhusu Maalim Seif wameamua kurudi tena ndani ya chama hicho.
Hata hivyo amesema kuna mipango ya hujuma inayofanywa na chama cha Act wazalendo kwa kuwatumia vijana wa CUF kwa kuwapa fedha ili kufanya maandamano yenye lengo la kumchafua Mwenyekiti wa chama cha CUF Prof Ibrahim Lipumba
Sambamba na hayo wamesema wao kama chama cha CUF wako tayari na watashirikiana na chama chochote chenye nia ya dhati ya kuiondoa CCM madarakani kwa kuachiana majimbo na sio kutafuta ruzuku.
Comments