KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B LAWASIMIKA 'VONGOZI WA MPITO'
KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B LAWASIMIKA WARITHI WA MAMA RWAKATARE KATIKA KIPINDI CHA ' MPITO'
Dar es salaam
Kanisa la Tanzania Assemblies of God 'Mlima wa moto mikocheni B'leo limewasimika vioongozi wawili wa kanisa hilo ambao wataliongoza katika kipindi cha mpito ikiwa ni siku chache tangu kufariki kwa aliyekuwa mchungaji wa kanisa hilo Dkt Getrude Rwakatare.
Akizunumza wakati wa tukio la uswimikaji wa viongozi hao mwanzilishi wa makanisa ya Calvary hapa nchini Askofu Dunstan Maboya amelitaka kanisa hilo kuendelea kuwa wamoja kwa kuendelea kuyaenzi yale aliyowaachia hayati Dkt Rwakatare kwa kuendelea kushirikiana na kuwa kitu kimoja.
Viongozi hao waliochaguliwa kwa kupigiwa kura ni pamoja ni Rose Mgeta na Willium Mwakitalu ambao wameahidi kulitumikia vyema kanisa hilo na madhabahu ya Bwana kwa kuwaunganisha kwa pamoja waumini wote.
Kusimikwa kwa watumishi hao wa Mungu kumehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa dini pamoja na watoto wa marehemu Mama Rwakatare na kunalifanya sasa kanisa hilo kuendelea na uongozi katika kipindi cha mpito ambacho viongozi hao watahudumu mpaka pale taarifa nyinginezo zitakapotolewa.

Comments