MAANDALIZI MAONYESHO YA SABASABA 2020 'YAPAMBA MOTO'



Dar es salaam.
Kuelekea maonyesha ya sabasaba Mamlaka ya  Maendeleo ya biashara Tanzania (TANTRADE) kupitia wizara ya viwanda na Biashara imesema imesajili asilimia 75%  ya makampuni 3600 yanayotarajiwa kushiriki katika  maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari  wakati akikagua maendeleo na maandalizi ya maonyesho hayo katika viwanja vya mwalimu nyerere [SABASABA]jijini Dar es salaam hayo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Eng. Stella Manyanya, amesema hatua hiyo ni mwernedo mzuri kuwa maonyesho hayo yatakuwa na mwitikio mkubwa 

''Ni  rai yangu kwa wafanya biashara na wanachi wote wanaotaka kutangaza biashara zao waje kujisajili na kupitia miongozo tunayopewa na Rais Magufuli, kuhakikisha tunawaendeleza wafanyabiashara na makampuni ya ndani ili wakue kibiashara  na kwa kuzingatia kwamba wafanya biashara wamepitai kipindi kigumu cha tishio la CORONA tumeweka punguzo  la ada kwa wafanya biashara wadogo na wakubwa "Alisema Eng Manyanya. 
                           Hata hivyo amesema , Maonesho hayo yataendeshwa chini ya muongozo maalumu ambao umetolewa na  wizara ya afya kuhakikisha tahadhari ya kujikinga na virusi vya COVID 19 inachukuliwa  watu watavaa barakoa na pia kutakuwa na vitakasa mikono.

"Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwajinsi ambavyo ametuwezesha kwa kiasi kikubwa kutukinga na janga la CORONA  ambalo lilikuwa ni tishio ambapo pengine hata tusingeweza kufanya maonesho mwaka huu na hata hapa TANTRADE tulitenga  kama  sehemu moja wapo ya kituo kwaajili ya wagonjwa  lakini tunamshukuru Mungu ameepesha na sasa kituo hiki sasa kinaendelea na shuguli zake za kibiashara"Alisema 

Katika hatua nyingine Waziri Manyanya amesema watajizatiti kuonesha maonesho kwanjia ya mtandao kwani kuna mazao kama mpunga na mahindi yamepatikana kwa wingi hapa mchini hivyo mazao hayo yatatangazwa kwa njia ya mtandao.

Pamoja na hayo Mhe.Stella amesema kutakuwa na mikutano kati ya wazalishaji na watu wateknolojia katika mazao hasa ya korosho,Kahawa,katani na mazao mengine mbalimbali hivyo kutakuwa siku ya kubadilishana mawazo kwa wafanyabiashara hao kati ya wazalishaji pamoja na watengenezaji wa teknolojia mbalimbali.

"Kutakuwa na onesho la kipekee litakalo kwenda kwa jina la mvinyo na Mkeka kwaajili ya kutangaza mvinyo inayotengenezwa hapa nchini njoo utakunywa mvinyo ukiwa umekaa kwenye mkeka "Alisema .
Mwamba wa habari ,tumezungumza na baadhi ya wananchi waliofika katika viwanja hivyo kujionea  maandalizi ya maonesho hayo ambapo wamesema kuwa  maonesho ya mwaka huu huenda yaka ni yakipekee (Babu kubwa kwa kutokana na unafuu wa punguzo kwa wafanya biashara utavutia wengi kuja kununua na kujioneo bidhaa mbali mbali .

"Mwaka huu ni mzuri sana kwa sabasaba kinacho pandishaga bei ya bidhaa ni kodi  na ada za meza  na mabanda  kwajinsi wanavyosema wamepunguza bei nnaimani hata biadhaa hazitauzwa  bei ghali  nawaomba wananchi wenzangu tufike kwa wingi  ,pia humu kunaburudani nyigi kuna mabembea ya watoto kuona wanayama ,pia kunakujifunza mbinu mbali mbali za ukulima ujasilia mali na ufugaji  "Alisema Mwanachi

Maonyesho ya kibiashara ya  kimataifa ya sabasaba hufanyika kila mwaka mwezi julai jijini Dar es salaam nchini Tanzania na kuhudhuriwa na wananchi pamoja na wafanyabiashara wakubwa,wakati na wadogo kutoka kote ulimwenguni.

Comments