NCCR YAWATAKA WANASIASA KUACHA 'KUJIVUNA'


Dar es salaam.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi Jams Mbati amewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini Tanzania kushirikiana pamoja  katika kuelekea uchaguzi mkuu ili nchi hiyo iwe salama.

Rai hiyo ameitoa mapema leo jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ... uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October mwaka huu.

Amesema kuwa, endapo vyama vyote vitakua na maamuzi sahihi katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu ikiwa bado nchi hiyo ipo katika mapambano ya ugonjwa wa Covid 19 basi Tanzania itakua ni sehem salama ya kuishi.

",Asilimia 96 ya majanga ya kitaifa yanasababishwa na kiburi cha binaadam kwa kujiona wao ni bora kuliko taifa, ubinasfi tumeueka mbele"amesema Mbatia.

Aidha ameongeza kuwa, NCCR ipo tayari kwa majadiliano au midahalo na chama chochote cha siasa nchini ili kuweza kufikia maridhiano ya pamoja ya kueka Tanzania sehemu salama.

"Endapo viongozi wote wa siasa nchini wataweza kutanguliza taifa kwanza bila kujiangalia wao basi tutaweza kufika mbali hata kupata katiba tunayoitaka"amesema Mbatia

Hata hivyo, ameitaka tume ya uchaguzi kufanya maamuzi sahihi bila kufuata shinikizo la chama chochote cha kisiasa ili kuweza kutenda haki katika uchaguzi mkuu.

Comments