TLP YASOMBA ZAIDI YA WANACHAMA 80 WA CHADEMA,JIMBO LA KIBAMBA


TLP YASOMBA ZAIDI YA WANACHAMA 80 WA CHADEMA,JIMBO LA KIBAMBA





Dar es salaam.

Chama cha Tanzania Labour Party [TLP]leo kimewapokea wanachama zaidi ya 80 waliojiunga na chama hicho kutokea chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.


Akizungumza wakati akiwapokea wananchama hao mwenyekiti wa Taifa TLP,Dkt Augustine Lyatonga Mrema amesema wanachama hao ni wa ngome ya vijana ya Chadema ambao wameamua kuachana na chama hicho na kujiunga na TLP kutokana na Chadema kukosa mwelekeo.

Wanachama hao ambao wanatokea jimbo la Kibamba wamejiunga na TLP ili kuendeleza juhudi za chama hicho kinachomuunga mkono Rais Dkt John Magufuli katika kasi yake ya kuliletea maendeleo taifa la Tanzania.

Aidha Dkt Mrema amesema kuwa Rais Magufuli anapaswa kuungwa mkono na kila anayelitakia mema Taifa la Tanzania hivyo kuondoka kwa wanachama wa Chadema jimbo la Kibamba na kujiunga na TLP ni dalili tosha kuwa Rais Magufuli anakubalika kila kona.

Hata hivyo chama hicho kimeongeza kuwa kitaweka wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani katika jimbo la kibamba na kina uhakika wa kushinda katika nafasi hizo na hatimaye kuingoa Chadema ambayo haijafanya maendeleo yoyote katika jimbo hilo tangu ilipochaguliwa.

Comments