Kanisa la mlima wa moto lakanusha wachungaji wake kufikishwa mahakamani,lasema halina tawi Buza.

Kanisa la mlima wa moto lakanusha wachungaji wake kufikishwa kortini,lasema halina tawi Buza.


Kanisa la Mlima wa Moto limekanusha taarifa iliyoripotiwa katika gazeti moja la kila siku nchini kufikishwa mahakamani kwa wachungaji wa kanisa hilo tawi la Buza, Bw Pecience Sunga na mkewe Bi,  Michou Sunga si wachngaji wa kanisa hilo.

Akizungumza makao makuo ya kanisa hilo Mikocheni Jijini Dar es salaam Mchungaji Kiongozi William Mwakitalu kwa niaba ya wachungaji wengine alisema wachungaji hao si watumishi wa Kanisa la mlima wa moto mikocheni B, 

"Napenda kutoa ufafanuzi kuhusu wachungaji walio ripotiwa kufikishwa mahakamani kuwa si watumishi wa kanisa Kanisa la mlima wa moto mikocheni B hivyo napenda kutoa pile kwa wale wote walioshtushwa na taarifa hii" Alisema Mchungaji Mwakitalu.

Alisema wachungaji wote makao makuu ya kanisa pamoja na matawi yote nchi nzima wapo salama hivyo watajwa katika taarifa hiyo si watumishi wala wachungaji wa kanisa hilo.

Mchungaji Mwakitalu ameyataka matawi ya kanisa hilo mkoa wa Dar es salaam kuwa ni Mlima wa moto Bunju B ambalo linasimamiwa na mchungaji  Sebastian Kimario, kanisa la mlima wa moto Boko ambalo linasimamiwa na mchungaji Gosbert Simtovu.

Amelitaja lingine ni kanisa la mlima wa moto Gezaulole kigamboni manalo linasimamiwa na mchungaji Dickson Masima hivyo wachungaji waliofkishwa mahakamani sio wa kanisa hilo.

Comments