FMJ HARDWARE KUFANYA MNADA WA VIFAA VYA UJENZI WA KIHISTORIA DAR

 FMJ HARDWARE  KUFANYA MNADA WA VIFAA VYA UJENZI WA KIHISTORIA DAR


Kampuni ya uuzaji wa vifaa vya ujenzi Fmj Hardware Ltd imewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika mnada mkubwa unaotarajiwa kufanyika August 31 mwaka huu kupitia mtandao ili waweze kupata bidhaa zenye ubora
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo, Fredrick Ally Sanga amesema kuwa mnada huo unakua na vifaa mbalimbali vya ujenzi ambapo unaweza kupata vifaa vyote kuanzia msingi hadi kupaua.

Amesema kuwa, wamekua na utaratibu wa kuuza vifaa vya ujenzi katika mnada mkubwa kwa njia ya mtandao kwa lengo la kuwafikia watu wengi zaidi na kuweza kupata manufaa makubwa sana kupitia mnada huo.

"Mnada huu utaanza Majira ya saa sita mchana ambapo umepewa jina la "Njoo upate Bei yako" kwa lengo la mtu yoyote atakae fika katika ofisi (duka) zetu zilizopo buguruni sheli mtaa wa kisiwani jijini Dar es Salaam ataweza kupata huduma kulingana na pesa yake"amesema Sanga.

Hata hivyo, amewataka wafanyabiashara nchi nzima kulipa kodi stahiki kwa Serikali ili iweze kuwatengezea mazingira mazuri ya kibiashara na kuwafungulia milango zaidi kwa masoko makubwa ya ndani na nje ya nchi. 

Ameongeza kuwa, wataendelea kushirikiana na Serikali kufanya uwekezaji mkubwa utakaoweza kupanua soko la ajira kwa watanzania

Hata hivyo kwa wananchi ambao wangependa kushiriki kwa   kununua bidhaa katika mnada huo wanaweza kuwasiliana na FMJ HARDWARE Kwa namba 0653  312438 ,0716902995

Comments