FMJ HARDWARE WAJA NA MNADA MKUBWA''NJOO UPATE BEI YAKO'' KUFUATIA TANZANIA KUINGIA UCHUMI WA KATI.

 FMJ HARDWARE WAJA NA MNADA MKUBWA''NJOO UPATE BEI YAKO'' KUFUATIA TANZANIA KUINGIA UCHUMI WA KATI.




DAR ES SALAAM.

Siku chache baada ya Tanzania kuingia uchumi wa kati,Kampuni ya usambazaji na uuzaji wa vifaa vya ujenzi [FMJ]ya jijini Dar es salaam inatarajia kufanya mnada mkubwa wa  uuzaji wa vifaa vya ujenzi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii uliopewa jina la 'NJOO UPATE BEI YAKO' ili kuwawezesha wananchi kupata huduma hiyo kwa haraka na kwa wakati zaidi.


Akizungumza na wanahabari kwa niaba ya wakurugenzi wa kampuni hiyo kubwa hapa nchini ya usambazaji na uuzaji wa vifaa vya ujenzi  meneja mauzo wa kampuni hiyo Fredrick Sanga amesema mnada huo   ambao utafanyika ikiwa ni awamu ya pili  umelenga kuwafanya wananchi wapate bidhaa bora za ujenzi wa nyuma,ofisi,shulu na viwanda kwa kutumia bidhaa bora za ujenzi na kwa gharama nafuu kuanzia hatua za awali za ujenzi mpaka hatua za umaliziaji wake  huku akiongeza kuwa njia hiyo itarahisisha upatikanaji rahisi wa vifaa vya ujenzi kwa 

’ndugu wanahabari mnada huu utafanyika mubashara yaani moja kwa moja kutoka hapa FMJ HARDWARE LIMITED buguruni kisiwani na hakika wateja watakaoufutalilia mnada huu watapata bidhaa bora kwa bei watakazochagua wenyewe’’ alisema Bw Sanga.

Aidha ameongeza kuwa kwa sasa wataendelea   kufanya mnada kupitia vyombo mbali mbali vya habari kufuatia  mnada ambao ulirushwa mubashara na vyombo vya habari na mwitikio wake ulikuwa ni mkubwa sana hali iliyowafanya kufanya awamu ya pili ya mnada huo.

Mnada huo unaotarajia kufanyika aagosti 31,2020 umekuja kwa mara nyingine ikiwa ni harakati za kampuni hiyo kuunga mkono juhudi za Rais Dkt John Magufuli katika kulijenga taifa na kulipeleka katika uchumi wa kati na utarushwa kupitia vituo vya habari vya mtandaoni vya  TanzaniteTV,AyoTV,GlobalTV ,Dar mpyaTV  Onliune na Icon TV


Hata hivyo kwa wananchi ambao wangependa kushiriki kwa   kununua bidhaa katika mnada huo wanaweza kuwasiliana na FMJ HARDWARE Kwa namba 0653  312438 ,0716902995








Comments