Skip to main content

RITA 'Mpango wa Usajili vyeti vya kuzaliwa watoto chini ya miaka 5 wa itangaza Tanzania Kimataifa'

 

Mpango wa Usajili vyeti vya kuzaliwa watoto chini ya miaka 5 wa itangaza Tanzania.

Serikali kupitia Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini kwa kushirikiana na wadau wengine inatekeleza Mpango wa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa usajili wa matukio muhimu ya Binadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Emmy Haudson amesema mpango huo unalenga kuhakikisha kuwa kila mtoto anaezaliwa anapata cheti cha kuzaliwa kwa muda mfupi baada ya tukio la kizazi kutokea.

Aidha ameongeza kuwa utekelezaji wa mpango huo unafanyika kwa kusogeza huduma karibu na makazi ya wananchi kwa kutoa huduma hiyo bila malipo katika ofisi za Watendaji Kata na vituo vya Tiba vinavyotoa huduma ya Afya ya mama na mtoto.

Aidha amesema kupitia mpango huo wamefanikiwa kusajili watoto zaidi ya milioni tano na u vyeti katika mikoa 18 ambayo mpango unatekelezwa na idadi hiyo kupandisha wastani wa watoto walio na vyeti vya kuzaliwa nchini kutoka asilimia 13 mwaka 2012 hadi asilimia 49.

Hata hivyo amesema mikoa ambayo mkakati wa usajili wa watoto unatekelezwa ni pamoja na Mbeya, Songwe, Mwanza, Iringa, Njombe, Geita, Shinyanga, Mtwara, Lindi, Mara, Simiyu, Dodoma, Singida, Morogoro, Pwani, Tanga na Kilimanjaro.

“Kupitia mafanikio hayo Tanzania imeweza kutambulika kama moja ya nchi inayopiga hatua katika usajili wa vizazi hata kuchaguliwa kati ya nchi 5 Barani Afrika na pekee kwa Afrika Mashariki kuwasilisha mada kuhusu mikakati na mafanikio ya usajili yaliyopatikana katika kipindi cha mlipuko wa homa kali ya mapafu (COVID 19)”Amesema Afisa Emmy.

Bi. Emmy amesema mpango wa usajili wa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano ni endelevu katika maeneo ambayo umeanza kutekelezwa hivyo wananchi katika mikoa tajwa waendelee kuitumia fursa hiyo kuwapatia watoto vyeti vya kuzaliwa mara tu wanapozaliwa.

Mamia Wajitokeza Kuilaki Treni Baada Ya Kuukosa Usafiri Kwa Kipindi Cha Miaka 34




Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi akiongea na Wananchi mara baada ya treni hiyo ya mizigo ikiwa na mabehewa 10 yenye tano 400 kuwasili katika stesheni ya Arusha mapema leo saa tano ikiwa ni safari ya majaribio kabla ya usafiri huo kuanza mwezi huu mwishoni picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha

Sehemu ya wananchi wakiingalia Treni mara baada ya kuwasili kwenye Stesheni ya Treni Jijini Arusha ikiwa ni safari ya kwanza baada ya miaka 34 iliyopita kusimama kwa usafiri huo jijini hapa
Wananchi waliofika kuipokea Treni ya mizigo ya majaribio kwenye hafla ya mapokezi leo jijini Arusha kama walivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha wakiilaki treni hiyo ikiwasili kwenye Stesheni ya Railway iliyopo Krokoni Kata ya Levolosi jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha
Wananchi wakifuatlia hotuba ya Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Arusha Mwita Zakaria kwenye hafla ya mapokezi ya Treni ya mizgo iliyowasili leo ikiwa ni safari yake ya kwanza baada ya miaka 34 kupita na kuanza tena kutoka huduma mwishoni mwa mwezi huu.
Sehemu ya Mabehewa kumi ya Treni hiyo ya mizigo kama yalivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha mapema leo katika Stesheni ya Reli iliyopo eneo la Krokoni kata ya Levolosi jijini Arusha
Baadhi ya wananchi wakipata fursa ya kupiga picha na usafiri huo wa Treni ikiwa ni sehemu ya hafla hiyo mara baada ya kuwasili katika stesheni ya reli iliyopo kata ya Levolosi jijini Arusha
 Umati wa wananchi na wakazi wa jiji la Arusha waliojitokeza kwenye hafla ya kuwasili kwa treni ya mizigo iliyowasili kwa mara ya kwanza baada ya kitambo kirefu kusimama kwa usafiri huo takribani miaka 34 iliyopita usafiri huo utaanza rasmi mwishoni mwa mwezi huu.

Na Ahmed Mahmoud Arusha
MAMIA ya wananchi jijini Arusha wamejitokeza kwa wingi kwenye hafla ya mapokezi ya Treni ya mizigo ya majaribio iliyowasili ikitokea Dar es salaam na mabehewa kumi ya Saruji yenye tani 400 na kupokelewa na Mkuu wa wilaya ya Arusha.
 
Akizindua hafla hiyo ya mapokezi ,mkuu wa wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi, amewaomba wananchi kuhakikisha wanailinda na kuitunza miundo mibinu ya reli ili iweze kudumu na kuwahudumia wananchi .
 
 Ametoa wito kwa wafanyabiashara kuitumia treni hiyo ya mizigo  kusafirishia bidhaa  zao  na hivyo kuwapa unafuu wa bei ya bidhaa na kuboresha maisha ya wananchi kama lilivyo lengo la serikali ya awamu ya Tano kuinua maisha ya watanzania.
 
Alisema kuwa ujio wa treni hiyo ya Mizigo ni mwanzo wa treni nyingine ikiwemo treni ya Abiria itakayosaidia kusafirisha na kushuka kwa bei za bidhaa ikiwemo saruji na usafiri wa Abiria kwa bei ya 18,000 badala ya elfu 30,000 hadi 35,000 kwa usafiri wa mabasi.

Aidha alisema kuwa treni moja itakuwa inapakia tani zaidi ya mia nane za Mizigo sawa na malori 80 na hivyo kusaidia kuokoa uharibifu wa barabara unaosababishwa na wingi wa malori ya Mizigo 

"Wananchi lindeni na kutunza miundombinu ya Reli ili isihujumiwe na kuturudisha katika zama za kale jambo ambalo tunatakiwa tuliona na kutoa taarifa kwa haraka katika kudhibiti matukio kama hayo"alisema Mkuu huyo

Awali mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro  aliyewasili na treni hiyo kutokea kituo cha Usariver wilayani Arumeru, hadi jijini Arusha alisema kwa mara ya kwanza  treni hiyo ya mizigo inatambulishwa  rasmi kwa wananchi  na huo ni mwanzo wa safari ya maendeleo na kuashiria kupokelewa kwa treni ya abiria ambayo itaanza mwishoni mwa mwezi huu wa Augosti 2020.
 
 Alisema serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na daktari John Magufuli, inatekeleza Ilani ya uchaguzi kwa vitendo na sio maneno na wananchi ni mashahidi.
 
 Muro, amewaomba wafanyabiashara kuituma fursa hiyo ya uwepo wa treni hiyo kusafirisha bidhaa za viwandani kutoka mikoa mbalimbali kuipeleka mkoani Arusha kutoka na kwenda mikoa mingine.
 
Akitoa salamu zake ,Katibu wa Chama cha Mapinduzi,wilaya ya Arusha, Denis Mwita, amesema  ujio wa treni hiyo ni kurahisisha huduma ya usafirishaji wa mizigo na kuwapunguzia gharama za mizigo na usafirishaji wananchi.
 
Alisema sasa Chama cha Mapinduzi kimefikia mwishoni mwa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020  ambayo imetekelezwa kwa vitendo na wananchi ni mashahidi kwa maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano ya awamu ya kwanza ya rais Magufuli.
 
Katibu mwita, alisema mkoa wa Arusha, una viwanda vingi ikiwemo vya mabati na chuma  lakini ni mkoa ambao hauna kiwanda cha Saruji hivyo treni hiyo itatumika kusafirishia pia Saruji kutoka kwenye mikoa mingine  inakozalishwa  na kuileta Arusha hivyo kupunguza gharama za bei za bidhaa na kuwataka wananchi kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi na serikali yake.
 
Aliwaambia wananchi kwamba hawana cha kumlipa rais Magufuli, kutokana na aliyoyafanya hivyo  wahakikishe wanamlipa kwa kumpatia kura za kutosha kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.
 
Baadhi ya wananchi waliokuwepo kwenye hafla hiyo wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwasogezea huduma hiyo ya usafiri na kuwapunguzia gharama za nauli kutoka kiasi cha 30.000 hadi Elfu kumi na nane

Comments