waziri Kigwangala azindua muhuri wa usalama wa wasafiri''SAVE TRAVELS''asema Tanzania imeaminiwa kuwa sehemu salama duniani kwa wasafiri
PICHA: Waziri Kigwangala Azindua Matumizi ya MUHURI wa Usalama wa Wasafiri Uliotolewa na Baraza la Wasafiri Na Utalii Duniani (WTTC)
Harakati za jiji 14 hrs ago
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki (wa tatu kutoka kushoto) na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi wakionesha nembo ya Muhuri wa Usalama kwa Wasafiri iliyotolewa kwa Tanzania na Baraza la Wasafiri na Utalii Duniani (WTTC) leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akizungumza wakati wa tukio la uzinduzi wa matumizi ya Muhuri wa Usalama kwa Wasafiri iliyotolewa kwa Tanzania na Baraza la Wasafiri na Utalii Duniani (WTTC) jijini Dar es salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ( katikati) akionesha nembo ya Muhuri wa Usalama wa wasafiri iliyotolewa kwa Tanzania na Baraza la Wasafiri na Utalii Duniani (WTTC) leo jijini Dar es salaam. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Diamond Platinum na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania, Richard Rugimbana.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki akizungumza wakati wa uzinduzi wa matumizi ya Muhuri wa Usalama kwa Wasafiri iliyotolewa kwa Tanzania na Baraza la Wasafiri na Utalii Duniani (WTTC) leo jijini Dar es salaam. Wengine wanaoonekana pichani ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania, Richard Rugimbana, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi na Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumza wakati wa tukio la uzinduzi wa matumizi ya Muhuri wa Usalama kwa Wasafiri iliyotolewa kwa Tanzania na Baraza la Wasafiri na Utalii Duniani (WTTC) leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ( katikati) akionesha nembo ya Muhuri wa Usalama wa wasafiri iliyotolewa kwa Tanzania na Baraza la Wasafiri na Utalii Duniani (WTTC) leo jijini Dar es salaam akiwa na Mwanamitindo Millen Magese na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania, Richard Rugimbana.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ( kulia) akisalimiana na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Harmonize (kushoto) wakati wa uzinduzi rasmi wa matumizi ya nembo ya Muhuri wa Usalama wa wasafiri iliyotolewa kwa Tanzania na Baraza la Wasafiri na Utalii Duniani (WTTC) leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ( katikati) akisalimiana na Mwanamuziki Zuchu wakati wa uzinduzi wa matumizi ya nembo ya Muhuri wa Usalama wa wasafiri iliyotolewa kwa Tanzania na Baraza la Wasafiri na Utalii Duniani (WTTC) leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania, Richard Rugimbana.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ( katikati) akifurahia jambo akiwa ameshika kijarida chenye nembo ya Muhuri wa Usalama wa wasafiri ambayo imetolewa kwa Tanzania na Baraza la Wasafiri na Utalii Duniani (WTTC) leo jijini Dar es salaam. Matumizi ya nembo hiyo yanaitambulisha Tanzania kuwa nchi salama kwa wageni mbalimbali hususani watalii wanaokuja kutembelea vivutio mbalimbali.
Comments