WORLD ISLAMI CALLSOCIETY YATOA MSAADA KWA WENYE ULEMAVU DAR ES SALAAM

     WORLD ISLAMI CALLSOCIETY YATOA MSAADA KWA WENYE ULEMAVU DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu.

Mkurugenzi wa jumuiya ya WORLD ISLAMIC CALL SOCIETY,, Ahmad Mus bah Almajlubu wa tatu kushoto  akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya walemavu waliopta msaada wa magongo ya kutembelea kutoka katika jumuiya hiyo wanne kulia kwake ni afisa ustawi wa jamii manispaa ya Temeke Bi Lilian Mafole .


Mkurugenzi wa jumuiya ya WORLD ISLAMIC CALL SOCIETY,, Ahmad Mus bah Almajlubu wa tatu kushoto  akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya walemavu waliopata msaada wa magongo ya kutembelea kutoka katika jumuiya hiyo .
Add caption

Mkurugenzi wa jumuiya ya WORLD ISLAMIC CALL SOCIETY,, Ahmad Mus bah Almajlubu wa tatu kushoto  akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya walemavu waliopata msaada wa  viti vya kutembelea[wheel chair]kutoka katika jumuiya hiyo .


baadhi ya walemavu wa macho wakifurahia jambo baada ya kupokea msaada wa fimbo za kuwaongoza kutoka katika jumuiya ya world islamic call society 

Mkurugenzi wa jumuiya ya WORLD ISLAMIC CALL SOCIETY,, Ahmad Mus bah Almajlubu akiwa kwenye picha yapamoja na mkurugenzi wa Dhahabu foundatio DKT Hadija Jilala

Add caption


Mkurugenzi wa jumuiya ya WORLD ISLAMIC CALL SOCIETY,, Ahmad Mus bah Almajlubu wa tatu kushoto  akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa taasisi ya dhahabu foundation pamoja na afisa ustawi wa jamii halmashauri ya Temeke


DAR ES SALAAM

Taasisi ya world Islamic call society imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa walemavu wilaya ya temeke ili kuwasaidia katika shughuli zao.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Ahmad Mus bah Almajlubu amesema wameamua kutoa msaada huo kutokana na kuguswa na maisha hao ili waweze kurahisisha maisha yao katika shughuli mbalimbali za kijamii.

Amesema kuwa,wataendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali zenye uhitaji wa kuwasaidia walemavu wenye uhitaji ikiwemo viti vya kutembelea(Wheel chair) magongo ya kutembelea pamoja fimbo kwa watu wasioona.

"Leo tumetoa msaada huu kwa walemavu 55,  taasisi hii ni ya kusaidia jamii hivyo haichagui dini kabila wala Taifa tunapenda kuguswa kwa kila mwenye tatizo"amesema Ahmad.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Temeke, Lilian Mafole ameishukuru taasisi hiyo kwa mchango mkubwa walioutoa kwa walemavu hao ambao utawasaidia kwa kiwango kikubwa.

"Walemavu ni wadau muhimu katika Maendeleo Serikali yetu inatambua mchango wao ndio maana wamewekwa katika ule mkopo wa halmashauri wa asilimia 10 ipo nafasi yao" amesema Mafole

Naye, Katibu wa wajasiri amali walemavu mkoa wa Dar es Salaam  David  Nyendo, amesema kwa sasa Serikali inatambua uwepo wao tofauti na hapo awali, hii ni kutokana kudai haki yao ndio maana walemavu wengi mjini wamejiajiri.

"Kwa sasa tukisema tunasikilizwa baada ya kudai haki yetu kwa muda mrefu, ni ngumu sana kumuelewa ombaomba mlemavu lakini hakuna anaependa kuwa vile tumebeba historia za huzuni mioyoni mwao, tunaishukuru sana taasisi hii kwa kutupa vifaa hivi"amesema...

Comments