WORLD ISLAMIC CALL SOCIETY KUENDELEZA MPANGO WAKE KUSAIDIA WASIOJIWEZA NCHINI.

WORLD ISLAMIC CALL SOCIETY KUENDELEZA MPANGO WAKE KUSAIDIA WASIOJIWEZA NCHINI


Jumuiya ya walinganiaji dini ya kiislam duniani(World Islamic call society) imesema itaendelea na mango wake wa kusaidia makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo walemavu, vikongwe pamoja na maskini wasiojiweza nchini Tanzania.


Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa jumuiya hiyo Tanzania, Ahmad Mas hab Almajlubu wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema jumuiya hiyo kwa sasa imerudi rasmi.

Amesema kuwa, jumuiya hiyo imejikita zaidi katika kusaidia watu mbalimbali wenye uhitaji maalum ambao wamekua na maisha duni kwa kuwachimbia visima vya maji Safi na salama, kujenga nyumba za ibada, madarasa pamoja na kutoa kutoa elimu ya lugha ya kiarabu.

" Jumuiya hii imeanzishwa mwaka 1984 na Makao makuu yake yanaatikana mjini Tripol nchini ambapo imejikita zaidi kuisaidia jamii katika kuwaendeleza kielimu kwa kutoa elimu ya ufundi (kushona) pamoja na komputer "amesema Ahmad.

Aidha amesema mbali na kutoa misadaa hiyo lakini pia imekua na utaratibu wa kuwapeleka nje wanafunzi bure waliomaliza kidato Cha nne na sita kwa lengo la kujiendeleza na elimu ya juu ili kujikwamua kimaisha.

Ameongeza kuwa, mpaka sasa wametoa misaada ya kuchimba visima, kutoa vifaa vya walemavu, kujenga misikiti katika mikoa ya  Dar es Salaam,Dodoma pamoja na Zanzibar.

"Licha ya mikoa hiyo, lakini pia tumekua na utaratibu wa kufururisha katika mikoa mingine pamoja na kutoa vifaa mbalimbali vya shule na madrasa sambamba kuitafsiri mas haf kwa lugha mbalimbali ikiwemo kiswahili"amesema Ahmad.

Comments