CHUO KIKUU,KATOLIKI RUAHA[RUCU]CHAWAASA WAHITIMU KIDATO CHA SITA 2020 KUCHAGUA VYUO VYENYE UBORA.

CHUO KIKUU,KATOLIKI RUAHA[RUCU]CHAWAASA WAHITIMU KIDATO CHA SITA 2020 KUCHAGUA VYUO VYENYE UBORA.

Dar es salaam
Na mwandishi wetu.
CHUO Kikuu Katoliki Ruaha (RUCU) kilichopo Mkoani Iringa kimesema Tanzania inahitaji wataalam wa afya ya Mazingira ili kuisaidia kufikia uchumi wa Viwanda.

 Kauli hiyo imetokewa jijini Dar es Salaam na afisa Uhusiano wa Chuo hicho Mwazarau Mathola wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 15 ya vyuo vya elimu ya juu,sayansi na teknolojia yanayoendelea katika viwanja vya mnazi moja jijini Dar es salaam

Amesema kuwa, tunahitaji wanafunzi wengi zaidi ambao wataweza kutusaidia katika kuchumi wa Viwanda na kuweza kutuelekeza Viwanda ambavyo vimekidhi vigezo. "Kwa mzazi au mwanafunzi ni vyema kujiunga na kozi ya Afya ya Mazingira kwani wataalam wa kozi hii ni wachache mno na wanahitajika sana Tanzania ambao wataweza kushauri hata eneo zuri la kujengea Viwanda " amesema Mwazarau.

 Aidha amesema kuwa, chuo hicho kina vitivo vinne ambavyo ni kitivo Cha Biashara, Kitivo cha  elimu,Kitivo cha Sayansi ya jamii,na Kitivo cha sheria pamoja na Taasisi moja ya masuala ya Afya.

 Ameongeza kuwa, Chuo kina uwezo wa kuwahudumia wanafunzi 5000, na kwamba mwaka 2020/21 Chuo kimelenga kudahili wanafunzi 3000 hadi 4000. 

Akizungumzia kozi ya ya afya ya mazingira amesema chuo hicho ni moja kati ya  vyuo viwili pekee vinavyotoa kozi hiyo hapa nchini huku hatua hiyo ikikifanya chuo hicho kuwa tofauti na vyuo vingine.

 Hata hivyo, amesema Chuo hicho kina  program ya Cheti (Astashada) 8, program za diploma (stashahada)10 , Digree (Shahada) 13, Masters 6 pamoja program ya Phd 1.

 Hata hivyo amewaasa wanafunzi pamoja na wazazi wanaopenda watoto wao kupata elimu bora kutembelea banda lao lililopo katika maonyesho hayo  ili kuweza kupata ushauri juu ya kozi gani wanazotakiwa kusoma katika vyuo vya elimu ya juu ikiwemo chuo cha [RUCU]

 Chuo hicho kipo Mkoani Iringa kilianza kikiwa chini ya Chuo Kikuu Cha mtakatifu Augustino [ SAUT] kikiitwa Ruaha University College[RUCO] na sasa ni Chuo Kikuu kinachojitegemea kutoka [RUCO] mpaka sasa kinatambulika kwa jina la  Ruaha Catholici  University [RUCU] Kwa kujua kozi zitolewazo na chuo hicho unaweza kutembelea website yao www.rucu.ac.tz . 



Comments