''MIMI NDO MGOMBEA NINAEYAJUA MATATIZO HALISI YA WANATEMEKE NICHAGUENI NIYATATUE''#ZAINAB MNDOLWA

''MIMI NDO MGOMBEA NAYAFAHAMU KERO NA MATATIZO YA WANATEMEKE NICHAGUENI NIYATATUE''#ZAINAB MNDOLWA.




Na Mwandishi wetu 

 Mgombea Ubunge Jimbo la Temeke kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Zainab Mndolwa amewaomba wananchi wa kata ya Sandali kuchagua ili awaletee maendeleo ambayo hayatajali itikadi za vyama vyao.

Bi Zainab ameyasema hayo katika mwendelezo wa kampeni zake katika kata ya Sandali, jimbo la Temeke jijini Dar es salaam
 
Aidha ameongeza kuwa endapo wananchi wa kata ya Sandali watamchagua basi hawatojutia maamuzi yao kwani yeye ndiye mgombea anayeyafahamu matatizo ya wakazi wa kata hiyo na jimbo lote la Temeke kiujumla na anaujua uongozi madhubuti kuwaongoza wanachi hao.

 Amesema kuwa,yeye ana kila sifa ya kua kiongozi bora kwani uongozi ameusomea darasani hivyo anajua kitu gani anakwenda kukiwakilisha bungeni. Aidha amesema kuwa, kiongozi ni jukumu kubwa hivyo lazima mtu awe na hofu ya Mungu kama unajiona huwezi kutekeleza ahadi bora uache kuliko kuwatesa wananchi kwa kutowasaidia matatizo yao. 

 "Bila kujali itikadi ya vyama vyenu naomba mnichague niwatumikie nitatue shida zenu kwani mna changamoto nyingi sana hapa Sandali ikiwemo kero ya barabara yenu ya sandali,kero ya kupata soko lenye miundombinu bora na za kisasa pamoja na ile ya watoto wenu kuchaguliwa shule za mbali pindi wanapomaliza darasa la saba na mtetezi wenu nimefika namkinichagua nitayamaliza hayo yote"amesema Zainab. 

 Hata hivyo, amesema kuwa, endapo atapewa ridhaa ya kuongoza Jimbo hilo basi atahakikisha anajenga barabara, vituo vya Afya,Soko pamoja na kuleta shule za Sekondari.

 "Ni lazima mufaidike na Kodi mnazozitoa na sio kuona Maendeleo sehem nyengine lazima tujenge barabara kila kata, vituo vya Afya pamoja na kujenga soko la uhakika"amesema Zainab. 

 Aidha amewaomba wananchi hao kumpigia kura nyingi za ndio mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof Ibrahim Lipumba pamoja na kuwachagua wagombea udiwani wote wa Jimbo hilo.

Comments