MGOMBEA UDIWANI KATA YA KISUKURU,LUCY LUGOME AAHIDI MAKUBWA KWA WAKAZI WA KATA HIYO

DAR ES SALAAM,

MGOMBEA UDIWANI KATA YA KISUKURU,LUCY LUGOME AAIDI MAKUBWA KWA WAKAZI WA KATA HIYO





 Mgombea wa nafasi ya udiwani kata ya Kisukuru wilayani Ilala jijini Dar es salaam Lucy Lugome amesema endapo wananchi wa kata hiyo watampigia kura na kumpa ushindi katika uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu atahakikisha anawaletea maendeleo makubwa.


Lucy amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni zake katika kata hiyo akisisitiza pia kuwainua wanawake kiuchumi endapo atachaguliwa kama diwani wa kata hiyo .


Hata hivyo ameongeza kuwa wanaake ndio msingi wa maendeleo hivyo atahakikisha anawainua kiuchumi ili kuijenga kisukuru madhubuti.

” Wanawake wenzangu ,Wanawake Tunaweza nawaomba mnichague Octoba 28/2020 ili niwe diwani wenu niwaletee maendeleo pamoja na Mbunge wetu Bonah Ladslaus Kamoli na Rais John Magufuli ambaye amewezesha nchi yetu kufikia uchumi wa kati “alisema Lucy.

Aidha Bi Lugome amewataka wanawake kujikwamua kiuchumi ili waweze kijishughulisha kwa sababu wanawake siku zote wanawaweza.

Amesema atawasimamia katika vikundi vya ujasiriamali na mikopo ya Serikali inayotolewa ngazi ya halmashauri hivyo aliwataka wanawake waandae katiba zao ili wasajili vikundi wale wasio sajili vikundi atashirikiana nao katika kuwasaidia uwandaaji wa Katiba.

Akielezea mikakati yake mingine amesema kata ya Kisukuru itakuwa ya kisasa kwa kusogeza huduma za jamii zote karibu na wananchi kwa kuwajengea vituo vya afya,soko ,kituo cha Polisi na viwanja vya michezo.

Aidha amesema wafanyabishara wa Bodaboda wote atawawekea utaratibu maalum watambulike kwa kusajiliwa ili waendeshe biashara zao kwa kufuata sheria na taratibu za nchi.

Amesema pia mikakati yake mingine atakapokuwa Diwani wa kata hiyo ni pamoja na  kutafuta maeneo ya viwanja vya michezo kwa vijana ili vitumike kwa matumizi mbalimbali  kimichezo.

''nayajua matatizo yote ya kata ya kisukuru na hakika mkinichagua nitawaletea maendeleo na kisukukru itakuwa ya kisasa tutajenga miundombinu ya barabara za mitaa hivyo msirudie makosa mliyoyafanya 2015 nichagueni niitekeleze vyema ilani ya CCM''alisema Bi Lugome

Kwa upande wake Mgombea ubunge Viti Maalum Mkoa Dar es salaam Janeth Masaburi amemwombea kura Rais wa Tanzania John Magufuli, mgombea ubunge Bonah Ladslaus Kamoli na diwani Lucy Lugome ili waweze kuletewa maendeleo.

Mama Janeth Masaburi amesena Magufuli ni jembe kiongozi anayesimamia maendeleo katika ukusanyaji mapato mpaka kuifikisha Tanzania hapa tulipo hivyo amewataka watanzania kuunga mkono juhudi zake kwa kumpigia kura kwa kishindo.

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Mstaafu wa Kibaha Assupter Mshama aliwataka wananchi wa Bonyokwa wamchague Lucy Lugome na Bonah Ladslaus Kamoli ili waweze kupata maendeleo kama umeme.

Comments