SHULE ZA BETHEL MISSION ZAWASHAURI WAZAZI KUCHAGUA SHULE ZENYE UBORA NA KUJENGA MAADILI MEMA KWA WATOTO.

<93tuma gmail.com=""> SHULE  ZA BETHEL MISSION ZAWASHAURI WAZAZI KUCHAGUA SHULE ZENYE UBORA NA KUJENGA MAADILI MEMA  KWA WATOTO.<93tuma gmail.com="">

<93tuma gmail.com="">


Dar es salaam
Na mwandishi wetu,
<93tuma gmail.com="">Wazazi na walezi wameshauriwa kuwapeleka watoto wao katika shule za Bethel Mission zilizopo mbezi Msakuzi na Ubungo, Makuburi jijini Dar es Salaam ili waweze kupata elimu bora na maadili mema.
<93tuma gmail.com="">
<93tuma gmail.com=""> Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa shule hizo, EMMANUEL MSHANA wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkakati wa shule hizo kuelekea katika mitihani ya Taifa ya darasa la nne na la saba mwaka huu.
<93tuma gmail.com="">
<93tuma gmail.com=""> Amesema kuwa, wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanafunzi wao wanafanya vizuri kitaifa licha shule kusimama takriban miezi mitatu wakati wa janga la Corona (Covid 19).
<93tuma gmail.com="">
<93tuma gmail.com=""> "Ni kweli shule zilisimama kipindi cha corona lakini baada ya Serikali kutangaza wanafunzi warudi shule June 29, tuliandaa hostel maalum ambazo ni kwa wanafunzi wanaojiandaa na mitihani darasa la nne na la saba"amesema MSHANA.
<93tuma gmail.com="">
<93tuma gmail.com=""> Aidha, ameongezea kuwa, hosteli hizo zimewasaidia sana wanafunzi kuweza kupata muda mwingi wa kujisomea ili kufidia muda waliokua nyumban.
<93tuma gmail.com="">
<93tuma gmail.com=""> "Hosteli hizi zinawasaidia wanafunzi kuamka alfajiri kujisomea na hata wakati wa jioni, hata siku za Jumapili wanafunzi hawa wamekua wakifundishwa kama kawaida, tunaamini wanafunzi wetu wamecover silabasi zote"amesema Mashana. Hata hivyo, amesema kipindi wanafunzi wapo nyumbani, shule hiyo iliweza kutengeza program maalum(Audio vision) ambayo walirekodi vipindi vya masomo manne na kuwarushia wazazi katika magroup WhatsApp ili watoto waweze kujisomea nyumbani.
<93tuma gmail.com="">
<93tuma gmail.com=""> "Katika mpango huu tumefanikiwa sana kwanza tumekua wabunifu mpaka sasa tumesharekodi vipindi vya masomo kwa wanafunzi wa darasa la saba na la nne, hata wanapokua likizo hii itawasaidia sana kuweza kujisomea"amesema MSHANA.
<93tuma gmail.com="">
<93tuma gmail.com=""> Amesema kuwa, kutokana na janga la Corona wazazi wengi walipata changamoto ya kushindwa kumalizia ada huku watoto wao wakikaribia kumaliza shule, lakini wameweza kukaa pamoja na kutoa mkataba wa kuwawezesha wazazi kumalizia ada hata wakiwa watoto wao wamemaliza shule.
<93tuma gmail.com="">
<93tuma gmail.com="">

<93tuma gmail.com="">

Comments