Vituo vya kutoa nafuu kwa waathirika wa dawa za Kulevya vyapata msaada.
Vituo vya kutoa nafuu kwa waathirika wa dawa za Kulevya vyapata msaada.
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imepokea msaada wa vifaa tiba vya kujikinga na magonjwa ya kuambukiza ikiwemo Corona pamoja na taulo za kike kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa dawa za Kulevya katika vituo vya methadone hapa nchini.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati akipokea msaada huo toka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) na Taasisi ya Flavian Matata Foundation, Kamshina Jenerali wa ( DCEA)James Kaji amesema pia Umoja wa Nchi za Ulaya kupitia mradi wake EU _ACT umetoa mashine 12 za kunawia mikono pamoja na sabuni zake kwa ajili ya vituo vya methadone hapa nchini.
Aidha amesema kwa upande wa Taasisi ya Flavina Matata imetoa taulo za kike kwa ajili ya Wanawake 35 ambao wanapata unafuu katika nyumba za upataji nafuu ili kuondokana na matumizi ya dawa za Kulevya.
Kamishana Kaji amesema Mamlaka hiyo katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kudhibiti vitendo hivyo kwa asilimia 90
Ameongeza kuwa mafanikio hayo yametokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi pamoja Taasisi hiyo kwa kufanya kazi kwa uthubutu na umakini mkubwa.
“Mafanikio haya yamesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa biashara ya dawa za Kulevya ambapo jumla ya vituo 9 vya methadone vimefuguliwa nchini” Amesema Kamishna Kaji.
Amesema vituo hivyo vimekuwa vikitoa tiba ya uraibu wa dawa za Kulevya ambapo jumla ya waathirika 8000 wamekuwa wakipata huduma kwa siku na wengine wakiendelea na kliniki.
Sambamba na hayo amesema jumla ya nyumba 29 za upataji nafuu(Sober house ) zimeazishwa ambapo Kati ya hizo 3 zimekuwa zikihudumia wanawake tu.
” Mamlaka yetu imekuwa ikifanya kazi kwa umakini na udhubutu mkubwa na hata shirika la umoja wa mataifa (UNODC) limekuwa likiitambua nchi ya Tanzania kama ni Moja ya nchi za mfano wa kuigwa katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za Kulevya” amesema Kamishna Kaji.
“Tunawapogeza sana kwa kujitoa kwa moyo mlioonesha kwa jamii ya waathirika wa dawa za Kulevya ni uzalendo wa kipekee”ameongeza
Kwa upande wake Mwanamitindo Flaviana Matata amesema kupitia Foundation yake wameamua kutoa msaada huo kwa ajili kuwasaidia wanawake ili waweze kujistiri .
Hata hivyo amesema Taasisi hiyo itatoa msaada huo kwa kipindi cha mwaka mmoja kama njia ya kuwasaidia wanawake na watoto wa kike.
Comments