''TANZANIA NDIYO NCHI YENYE TUME HURU YA UCHAGUZI BARANI AFRIKA''MCHUNGAJI ANTHONY LUSEKELO
Mchungaji wa kanisa la Maombezi GRC jijini Dar es Salaam Anthony
Lusekelo maarufu kama mzee wa
upako amewataka vijana kujiepusha na
vurugu ambazo zitahatarisha amani ya Tanzania kabla na baada ya uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika October 28 mwaka huu.
Rai hiyo ameitowa jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na
waandishi wa habari,ambapo amesema vijana wanatakiwa kuendeleza misingi ya
amani iliyoasisiwa na mababu zao ambao ni waasisi wa Taifa.
Amesema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa ambao wamekua
wakiwadanganya wananchi kuwa Tume ya uchaguzi (NEC) sio huru,jambo ambalo siyo
la kweli kwani barani Afrika,Tanzania pekee ndio nchi yenye Tume huru ya
uchaguzi.
"Tume ya Taifa ya uchaguzi Tanzania ni huru ndio maana
wagombea walikua na imani nayo ndio maana wakachukua fomu ya kushiriki
kugombea, ila ikitokea mgombea ameshindwa ndio anaanza kusema Tume sio
huru"amesema Mzee Lusekelo.
Hata hivyo, amesema kuwa Tanzania ni bora kuliko chama chochote
Cha siasa hivyo, watanzania wanatakiwa kuepuka kutumika vibaya katika
maslahi yao binafsi.
Aidha, amewetaka viongozi wa dini kuacha tabia ya kuwashawishi
waumini wao kuchagua mgombea wa chama fulani na badala yake waache waumini hao
kufanya maamuzi ili kuepusha kuwa makundi na mganyiko katika nyumba za ibada.
Comments