WAGOMBEA UBUNGE,ACT WAZALENDO WASEMA HAWATAMNADI LISSU,WAWATAKA WANACHAMA KUMPUUZA MAALIM SEIF NA ZITTO

 WAGOMBEA UBUNGE,ACT WAZALENDO WASEMA HAWATAMNADI LISSU,WAWATAKA WANACHAMA KUMPUUZA MAALIM SEIF NA ZITTO



DAE ES SALAAM,

Wagombea wa nafasi ya ubunge kwa tiketi ya  chama Cha ACT Wazalendo wamewataka wanachama wa chama hicho kuendelea kumuunga mkono mgombea wao wa Urais Bernad Membe.


Wakizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, mgombea ubunge wa Jimbo la Kibamba jijini Dar es salaam Mwesigwa Zaidi amesema kuwa, kufuatia kauli za Mwenyekiti wa chama hicho alizozitoa hivi karibuni, Maalim Seif Shariff Hamad kwamba kinamuunga mkono mgombea wa CHADEMA Tundu Lissu kauli hiyo inakiuka katiba ya chama hicho.

Amesema kuwa,kilichofanywa na Mwenyekiti wa chama hicho pamoja na Kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe si matakwa ya chama bali ni njama za viongozi hao,kwani kuna taarifa kwamba viongozi hao wamenunuliwa.

Ameongeza kuwa, Chama cha ACT sio cha zitto Kabwe wala Maalim Seif Shariff bali ni mali ya wananchi ambao ni wanachama wote, hivyo kwa mujibu sheria ya vyama vya siasa na katiba ya chama hicho viongozi hao sio wanachama tena wa chama hicho na wamepoteza sifa za luendelea kuwemo ndani ya chama.

Kwa upande wake, mgombea ubunge wa Jimbo la Kyerwa Ntareyelguru Juvenary Fredrick amesema kuwa, wao kama wabunge wa chama cha ACT Wazalendo hawapo tayari kumuunga mkono Tundu Lissu na kumuacha Mgombea aliyesimamishwa na Chama chao Bernard Membe ambaye wanaamini atashinda uchaguzi.

" Zitto Kabwe na Malim Seif Shariff Hamad wanachokifanya ni kinyume na sheria kwani, na sisi kama wabunge msimamo wetu hatutomnadi Tundu Lissu  na tunawaomba wanachama wetu nchi nzima kumpigia kura mgombea wetu"amesema Ntareyelguru

Ameongeza kuwa,
"Sisi tunajua haya yote yanayoendelea kua ni fitina walimtaka mgombea wetu achangie shilling billion moja kwenye kampeni za mgombea Urais wa CHADEMA ndio maana yametokea yote haya, nawashangaa kweli viongozi wetu"amesema Ntareyelguru

Aidha kwa upande mwingine wagombea ubunge hao wamesema kuwa watafungua kesi mahakamani ili sheria iangalie ni namna gani viongozi wa chama hicho walivyokiuka katiba ya chama chao na kupoteza sifa ya kuendelea kuwemo ndani ya chama.


Comments