''Chama bado ni mchezaji wetu hadi 2022''MO DEWJ


Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya wekundu wa msimbazi SIMBA,Mohamed dewj maarufu kama MO amekanusha tetesi zilizokuwa zimesamba katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habasi kuwa huenda mchezaji wa timu hiyo Clotus Chama akatimkia kwa mahasimu wao Yanga.


MO ameyasema hayo alipozungumza na wanahabari juu ya masuala mbalimbali ya timu hiyo.


Ameongeza kuwa Chama ataendelea kuitumikia klabu hiyo baada ya kusaini mkataba unaomalizika mwaka 22022.


Aidha akizungumzia tetesi za kutaka kumsajili mchezaji wa klabu ya Yanga,Mukoko Tonombe amesema wao kama klabu hawajawahi kuzungumzia suala la kutaka kumsajili mchezaji huyo na wala hakuna mpango huo kwani wamempa kocha wao jukumu la kujua ni mchezaji gani anayemtaka ambaye ataifaa timu hiyo na kwa wakati gani.

Comments