DAWOODI BOHRA TANZANIA WASHEHEREKEA MIAKA 77 YA KUZALIWA KWA KIONGOZI WAO DUNIANI.

waumini wa madhehebu ya dawoodi bohra Tanzania wakiwa katika matembezi ya amani kusheherekea miaka 77 ya kuzaliwa kwa kiongozi wa madhehebu hayo duniani,Dr Syedna Mufaddal Saifuddin jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.





Na mwandishi wetu,

Dar es salaa.

Jumuiya ya Dawoodi Bohra nchini Tanzania imeadhimisha siku ya kuzaliwa kiongozi wa madhehebu hayo duniani Dr Syedna Mufaddal Saifuddin kutimiza miaka 77 ambapo katika sherehe hizo ziliambatana na matembezi ya waumini wa madhehebu hayo yaliyoongozwa na brass band ya jeshi la magereza hapa nchini.

 Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam wakati wa matembezi hayo ya amani yaliyofanywa na jumuiya hiyo mwishoni mwa wiki mjumbe wa sherehe hizo HATIM DAUDI amesema kuwa jumuiya ya dawood bohras itaendelea kusisitiza  upendo na kusaidia wenye mahitaji ikiwemo chakula kwa wenye njaa hivyo sherehe za kutimiza miaka 77 kwa kiongozi wao wa dunia zitadumisha upendo,ushirikiano na amani.

''ndugu wanahabari sherehe hizi za kutimiza miaka 77 kwa kiongozi wetu mkuu wa jumuiya ya mabohora duniani zitaenda sambamba kwa kushikamana na yale ambayo pia yameelezwa na mtume Muhamad  na pia kusheherekea ushindi mnono wa rais wa taifa letu Dkt John Magufuli na tunampongeza sana kwa kutuongoza vyema na tunamwombe afya njema''alisema Hatim.

Naye mjumbe wa kamati tendaji wa jumuiya hiyo SAIFUDDIN JAMALEE amesema ametoa pongezi kwa Tanzania kuendelea kuwa nchi ya amani na kuwataka watanzania waendelee kuitunza amani tuliyonayo huku akitoa pongezi kwa jinsi serikali ilivyoshughulikia janga la corona na hatimaye kuifanya Tanzania kuwa nchi pekee inayosheherekea miaka 77 kwa kukusanyika na kufanya matembezi huku nchi nyingne zikishindwa kufanya hivyo kutokana na janga la virusi vya corona (covid 19).

Dawood bohra ni jumuiya ya kiislam inayoishi katika zaidi ya nchi 40 duniani ikiwemo Tanzania na ni jumuiya yenye wasomi wengi katika fani mbalimbali na wanaamini katika kupunguza njaa,kutunza mazingira na uoto asilia,usawa wa kijiunsia sambamba na kuitunza amani. 


waumini wa madhehebu ya dawood bohra Tanzania wakiwa katika matembezi ya amani kusheherekea miaka 77 ya kuzaliwa kwa kiongozi wa madhehebu hayo duniani,Dr Syedna Mufaddal Saifuddin















picha baadhi ya viongozi wa dawoodi bohra wakifurahia jambo katika  kusheherekea miaka 77 ya kuzaliwa kwa kiongozi wa madhehebu hayo duniani,Dr Syedna Mufaddal Saifuddin jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.






Comments