Kongamano la kisayansi la magonjwa yasiyo ya kuambukiza lafunguliwa Dar es salaam


Magonjwa yasiyoyakumbukiza yamelisababishia Taifa hasara kubwa kwa kuondoa nguvu kazi na kurudisha nyuma maendeleo ya mtu binafsi na Taifa kwa ujumla.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya katika ufunguzi wa Kongamano la pili la Kisayansi la maadhimisho ya wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza.
Akizungumza katika Kongamano hilo Prof. Makubi amesema asilimia 33 ya vifo vyote nchini kwa mwaka 2017 vimetokana na magonjwa yasiyoyakuambukiza ikiwemo magonjwa ya moyo na shinikizo la Damu kwa asilimia 13, Kisukari asilimia 2, saratani asilimia 7 na ajali asilimia 11.
Aidha amesema hali hiyo haikubaliki hivyo wanapanga mikakati ya pamoja ili kukabiliana na changamoto hiyo ambayo inaongeza utegemezi sugu kwa familia na kuongeza mzigo mkubwa kwenye mfumo wa afya kwa kuwa ni magonjwa ya muda mrefu na yanatumia rasilimali nyingi.
Hata hivyo amesema kupitia Kongamano hilo serikali inatarajia kupata mapendekezo ya wadau wa Afya ili kuweza kuimarisha huduma za kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza hivyo ni vyema yawe mapendekezo ya kutekelezeka.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya Dkt.Grace Magembe amesema kwa takribani miaka nane magonjwa yasiyoyakuambukiza yamekuwa yakiongezeka ikiwa ni pamoja na gharama za matibabu.
Aidha ameongeza kuwa lengo la Kongamano hilo ni kutoa uelewa kwa jamii kuhusu magonjwa hayo na njia za kukabiliana nayo ambapo katika wiki ya maadhimisho watatoa elimu kupitia sehemu mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari pamoja na kutoa huduma ya upimaji katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyoyakuambukiza yanachangia zaidi ya vifo milioni 41 ambayo ni sawa na asilimia 71 ya vifo vyote milioni 57 vilivyotokea mwaka 2016 huku mataifa ya Uchumi wa kati na chini kama Tanzania yakionekana kua

Comments