MANISPAA YA ILALA YAJIVUNIA ONGEZEKO LA MAKUSANYO YA KODI,YATOA VYETI KWA WALIOFANYA VIZURI KATIKA ULIPAJI KODI.

 

MANISPAA YA ILALA YAJIVUNIA ONGEZEKO LA MAKUSANYO YA KODI,YATOA VYETI KWA WALIOFANYA VIZURI KATIKA ULIPAJI KODI.




Dar es salaam

Ili kuendelea kuelimisha jamii na kuwafanya wafanyabiashara na wajasiriamali walipe kodi kwa wakati na kwa uaminifu Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam imetoa vyeti kwa wafanyabishara na wajasiriamali waliofanya vizuri katika kulipa kodi kwa wakati ambayo imewezesha kuvuka malengo ya ulipaji kodi kutoka shill 


Akizungumza katika hafla ya utoaji vyeti hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng'wilabuzu Ludigija amesema kodi hizo zimesaidia katika kuendesha miradi mikubwa ya kimaendeleo pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi. 

"Nawapongeza sana nyie mmeendelea kuwa walipakodi nb wazuri na Ili maendeleo yaweze kupatikana ni lazima wafanyabiashara walipe kodi kwa wakati bila shuruti, hivyo endeleeni kuwa mabalozi kwa wafanyabiashara wengine ili tuweze kupata mafanikio makubwa zaidi kwani zoezi hili litakuwa endelevu" Amesema Ludigija.


Aidha Katikb hatua nyingine amewashukuru wafanyabiashara katika Manispaa hiyo kwa  kuona umuhimu wa kulipa kodi kwa Serikali ili iweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi na ameahidi kuwa watahakikisha wanazitumia fedha hizo kutatua matatizo yote ya watanzania.Hata hivyo, amewataka wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanapolipa kodi katika mamlaka husika ili kuepuka kutapeliwa na kuingia kwenye migogoro na Manispaa ikiwemo kulipa faini.


Aidha kwb upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumane Shauri amesema kuwa, mwaka 2019 walitarajia kukusanya shi bill 57 lakini kutokana elimu inayotolewa na Manispaa hiyo wamevuka malengo na kukusanya sh Bill 58 sawa na asilimia 103.


Hata hivyo ameongeza kuwa, kutolewa kwa vyeti hivyo kwa wafanyabiashara  vitakua chachu ya kuleta Maendeleo na uzalendo kwa wananchi kwani Maendeleo ya nchi hiyo yataletwa na wafanyabiasha wote.Aidha amesema kuwa, Manispaa hiyo imejipanga vizuri katika kuhakikisha wafanyabiashara wote wanalipa Kodi na hakuna atakaekwepa, na ikibainika hatua za kinidham zitachukuliwa dhidi yao.

Naye, Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo,Turusubya Kamaramo, amesema kuwa,Manispaa ya Ilala kwa miaka 3 kutoka 2017/19 imevuka malengo ya kukusanya Kodi kutoka Sh Bill 46 hadi kufikia sh Bill 57 sawa na asilimia 10 huku kwa mwaka 2020/21  wanatarajia kukusanya sh Bill 60.Aidha amesema kuwa, wanatarajia kuandaa mpango kazi kwa mapungufu yote walioyagundua kutoka kwa wafanyabiashara ili kuweza kufikia malengo ya kukusanya sh Bill 100 kwa mwaka 2020/25 na kutoa hamasa kwa wafanyabiashara wengine waweze kulipa kodi.

Comments