[TIRA] YATAKIWA KUWEKA MKAKATI MADHUBUTI,SEKTA YA BIMA KATIKA KUKUZA PATO LA TAIFA KUFIKIA MWAKA 2030.
[TIRA] YATAKIWA KUWEKA MKAKATI MADHUBUTI,SEKTA YA BIMA KATIKA KUKUZA PATO LA TAIFA KUFIKIA MWAKA 2030.
Na mwandishi wetu,
Dar es salaam.
Menejimenti ya Mamlaka ya usimamizi wa shughuli za Bima Tanzania (TIRA) na wafanyakazi wake wametakiwa kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kuwa sekta ya bima inaongeza mchango wa pato la Taifa, kutoka asilimia 0.53 hadi kufikia asilimia 3 ifikapo mwaka 2030 kama mpango mkuu wa serikali unavyotaka.
Wito huo umetolewa mapema leo Jijini Dar es Salaam na kamshna wa bima hapa nchini Dkt Mussa Juma wakati alipokuwa akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa mamlaka hiyo uliofanyika katika ukumbi wa benki kuu ya Tanzania ambapo amesema Mamlaka hiyo inatakiwa kufanya kila jitihada kuhakikisha mchango huo unafika asilimia 3 kufikia mwaka 2030.
Dkt Juma ameongeza kuwa kama mchango wa Sekta ya bima utafikia asilimia 3 kwenye Pato la Taifakufikia mwaka 2030 hatua hiyo itakuwa na matokeo chanya, hususan kwenye eneo la kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, ufugaji, uvuvi na misitu hivyo mamlaka ya usimamizi wa bima nchini.
Aidha ameongeza kuwa , sekta ya bima kuwa dumavu kunasababishwa na ushiriki mdogo wa watu au umma kwenye shughuli za bima, kwa sababu wananchi wengi hawana elimu ya kutosha ya masuala ya bima,hivyo ameitaka TIRA mpaka kufikia 2030 kuwajengea uelewa wananchi kufikia asilimia 80 kwenye masuala ya bima ili sekta hiyo iwe na mchango mkubwa hapa nchini.
"Ndugu wajumbe ninawakumbusha na nitaendelea kuwakumbusha, nguvu kubwa ielekezwe kwenye eneo la kuwafikia wasiofikiwa, menejimenti ya TIRA, wafanyakazi pamoja na wadau mnatakiwa kuongeza kasi ya kutoa elimu kwa umma ili kuweza kufikia asilimia 50 watu kuweza kutumia bima "amesema Dkt Mussa
Hata hivyo kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi idara mipango kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Theresia Henjewele amesema kuwa sekta ya bima ina mchango mdogo katika pato la Taifa hivyo yafaa sekta hiyo kutiliwa mkazo ili kuongeza tija kwa Taifa.
Aidha ameitaka Taasisi hiyo kujadili kwa pamoja katika vikao vyao na kufanya mipango ya kuyafikia malengo yao ndani ya miaka 10 ili kufikia asilimia 3 ya uchangiaji katika pato la Taifa lenye kuleta tija katika maendeleo ya nchi na sekta ya bima nchini.
Comments