Dar es salaam.
Kwaya ya mtakatifu Maria Consolata ya chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo -SUA kilichopo mkoani Iringa inatarajia kuzindua albam yake inayokwenda kwa jina la 'mpeni bwana utukufu'.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,mratibu wa kwaya hiyo Fredy Joseph amesema kuwa albam hiyo inazinduliwa ikiwa na lengo la kumtukuza mwenyezi Mungu sambamba kuelimisha jamii hasa vijana katika masuala mbalimbali katika jamii.
Amesema kuwa albam hiyo itakuwa na nyimbo kumi ambazo zimebeba maudhui ya kumsifu Mungu,kuitunza amani ya Taifa na kuhamasisha vijana kufanya kazi kwa bidii ikiwemo za kilimo pamoja na kuheshimu wazazi na jamii kwa ujumla.
''sisi kama kwaya ya mtakatifu MariaConsolata-SUA tumeamua kuja na albam hii ya Mpeni Bwana utukufu na ujumbe wa nyimbo hizi utapatikana pia kama miito katika mitandao mbalimbali ya huduma za simu hivyo nawaomba watanzania tutoe ushirikiano kwa kununua albam hii''amesema Fredy.
Aidha kwa upande wake mwenyekiti ya kamati ya uzinduzi wa albam hiyo George Africanus ameongeza kuwa uzinduzi wa albam hiyo unatarajiwa kufanyika disemba 19 mwaka huu katika ukumbi wa spiritant formation center uliopo jijini Arusha na itagusa watu wote bila kujali rika na dini zote hivyo amewaomba makampuni ya uuzaji na usambazaji wa kazi za wasanii kujitokeza ili kusambaza albam hiyo kote nchini.
''Albam hii itapatikana kupitia flasha na DVD lakini pia itapatikana katika platform zote za mitandao ya kijamii na internet na tumeandaa nyimbo kwa kila mtu ili hata kama mtu atafanya kazi kwa bidhi ajue anamtukuza Mungu na kuitunza amani yetu ambayo ni tunu ya taifa letu' amesema George.
Kwaya ya mtakatifu Maria Consolata ni kwaya ya wanafunzi wa chuo kikuu cha sokoine cha kilimo -SUA kilichopo mkoani Iringa.
|
|
Comments