MBUNGE JIMBO LA LUDEWA KUANZA KUTEKELEZA AHADI ZAKE,AKUTANA NA WANALUDEWA WAISHIO DAR ES SALAAM.

MBUNGE JIMBO LA LUDEWA  KUANZA KUTEKELEZA AHADI ZAKE,AKUTANA NA WANALUDEWA WAISHIO DAR ES SALAAM.

Mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akizungumza na Wana Ludewa waishio Jijini Dar es Salaam (hawamo pichani) kwaajili ya kuwaeleza Mambo mbalimbali yahusuyo Maendeleo ya Jimbo hilo.



DAR ES SALAAM.

Wito umetolewa kwa wana Ludewa wote waishio nje ya Ludewa Mkoa wa njombe kuungana kwa Pamoja katika kuleta Maendeleo katika wilaya yao.

Wito huo umetolewa Disemba 5,2020 Jijini Dar es salaam na Mbunge wa Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe  Joseph Kamonga wakati wa kikao cha Pamoja na wana Ludewa waishio Jijini Dar es salaam.

Kamonga amesema wanatakiwa waungane na kuwa kitu kimoja kama ilivyo kwa watu wa maeneo mengine ili kuweza husaidia kasi ya mendeleo Katika maeneo yao kwani kwa kufanya hivyo kutawafanya kuwa kitu kimoja katika kuleta maendeleo.

KAMONGA amewaahidi kuwa hatokuwa na makundi na matarajio yake na shahuku yake ni kuona wana Ludewa wanakuwa kitu kimoja katika swala zima la kuleta maendeleo katika wilaya hiyo.

"katika utelelezaji wa majukumu yangu nitasimamia ilani ya Chama cha Mapinduzi, lakini pia kauli Mbiu yangu nitakayoisimamia katika katika utekelezaji wa majukumu yangu ni Umoja na Kazi kwa maendeleo ya Ludewa" Amesema Mhe, Kamonga.

Ameongeza kuwa anazitambua changamoto mbalimbali zilizopo wilayani humo ambapo changamoto kubwa zaidi ni miundombinu ya  barabara Kama vile barabara inayoanzia kigasi mapogolo milo,na kuelekea ludende na barabara inayoanzia Muhoro inakuja ludende kwenda mkongobaki mpaka lugalawa zinatatizo kubwa.

"Barabara hiyo inategemewa sana na wananchi wa ludende kwa sababu kuna mazao mengi ya chakula na ya biashara, hata Serikali uzitumia kupeleka huduma za jamii na kukutana na changamoto hizo" ameongeza.

Aidha Amesema kuwa endapo kutaboreswa miundombinu ya barabara hizo kutasaidia kuinua Sekta ya kilimo ambayo itainua uchumi wa jamii na Taifa kwa ujumla.

"Serikali inawajibu wa kuhakikisha jamii inaishi bila ya kuwa na changamoto zinazoikabili hivyo nitahakikisha changamoto hizo na hasa zinazohusu barabara zinatatuliwa na tayari nimeshaanza mchakato wa kupeleka taarifa zake Serikalini" Amesema Kamonga.


Wananchi mbalimbali wenyeji wa Ludewa waishio Jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mbunge wao Joseph Kamonga (hayumo pichani) Katika mkutano wao wa pamoja na Mbunge huyo Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya Wananchi wa Ludewa waishio Jijini Dar es Salaam wakipiga picha na Mbunge wao Mhe. Joseph Kamonga (wa kwanza Kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao na Mbunge huyo uliofanyika Disemba 5 Katika  ukumbi wa mikutano wa hotel ya Rombo Green View iliyopo Sinza  Jijini Dar es Salaam.

Comments