TGNP MTANDAO YAADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA,WADAU WAPEWA NENO.
TGNP MTANDAO YAADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA,WADAU WAPEWA NENO.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda(picha na tgnp mtandao) |
Dar es salaam
Ikiwa ulimwengu unaadhimisha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,kuanzia november 25 hadi desemba 10 kila mwaka,Wito umetolewa kwa
wadau
mbalimbali nchini wametakiwa kutumia mpango kazi ulioandaliwa na Serikali
wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ili kutoa
elimu kwa jamii na kuhamasisha kutoa taarifa na kuzitunza kwa watu
wanaofanyiwa vitendo vya ukatili.
Wito huo umetolewa
jijini Dar es Salaam na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Anne Makinda wakati alipokua katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yenye (muktadha miaka 25 ya Being) ambapo kauli mbiu ya
maadhimisho hayo ni wekeza, wezesha tokomeza ukatili wa kijinsia.
Amesema kuwa, wadau
mbalimbali wa kupinga vitendo vya ukatili wanapaswa kueka kumbukumbu (taarifa)
za Matukio ya ukatili yanaporipotiwa ili vizazi vijavyo viweze kusoma na
kujinza mambo mbalimbali ambayo yalitokea na hatua zilizochukuliwa katika
kupinga vitendo vya ukatili.
"Nasisitiza tena
naomba muzitunze taarifa zenu ambazo mnazifanya katika kutokomeza ukatili wa
kijinsia zidi ya wanawake na watoto kwani Tanzania hatuna utaratibu wa
kuhifadhi kumbukumbu za Matukio"amesema Makinda.
''Kama kauli mbiu inavyotuongoza, suala
la kutokomeza ukatili wa kijinsia ni jukumu la kila mmoja katika nafasi yake.
Kauli mbiu hii inatupa msukumo wa kuhakikisha kuwa kila mmoja katika nafasi
yake anapaza sauti na kuchukua hatua ya kuzuia na kutokomeza vitendo vya
ukatili wa kijinsia katika maeneo mbalimbali ikiwemo nyumbani, kazini, katika
taasisi za elimu, katika ngazi ya jamii na serikali''amesema Makinda
Ameongeza kuwa Kutokomeza ukatili wa kijinsia ni kulinda haki za
binadamu. Tunapaswa kutambua kuwa wanawake na watoto pia ni binadamu hivyo,
haki zao ni haki za binadamu ambazo zinapaswa kuheshimiwa na kulindwa.
Tukumbuke kuwa tunapoangalia mustakabali wa taifa letu, ni wazi kuwa suala la
kutokomeza ukatili wa kijinsia ni kipaumbele. Taifa lisilo na ukatili wa
kijinsia ni taifa lenye maendeleo jumuishi, ya kasi na endelevu.
Ili kuwa na maendeleo endelevu kwa wote (Wanawake na wanaume) ni
lazima kuzingatia na kuheshimu haki za binadamu. Binadamu yeyote ili aweze kushiriki
kikamilifu katika shughuli za maendeleo ni lazima awe huru au asikumbane na
vitendo vya ukatili. Hivyo basi, usalama wa wanawake na watoto dhidi ya
vitendo vya ukatili wa kijinsia ni jambo la msingi sana kwa maendeleo na ustawi
wa taifa lolote.
Naye, Mkurugenzi wa
TGNP Mtandao Lilian Liundi amesema kuwa, kila mtu akisimama kwa nafasi yake
kupinga ukatili wa kijinsia Tanzania itaweza kupunguza vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa takwimu
zinatolewa kila mwaka kuhusu hali ya ukatili nchini lakini bado hakuna
uwajibikaji wa moja kwa moja, ndio huku akitoa mifano hai ambayo
imeshatokehasa suala la kwa watoto kukatishiwa ndoto zao kwa kufanyiwa ukatili.
"Serikali yetu
imejitahidi, kuweka sheria, sera na mikakati ya kutokomeza Ukatili wa Kijinsia
kwa wanawake na watoto lakini changamoto ilinayofifisha jitihada hizi ni bajeti
kidogo inayotengwa kuviwezesha vyombo husika. Tunaiomba serikali kuu na halmashauri
zetu, zitoe kipaumbele kwenye bajeti zake katika kuwezesha dawati la Jinsia na
mtoto polisi, kamati za Utekelezaji wa Mpango kazi wa Kutokomeza Ukatili kwa
Wanawake na watoto (MTAKUWWA) kuanzia ngazi ya Halmashauri hadi vijiji"
Lilian Liundi
Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Lilian Liundi |
Kwa upande wake,
Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto Delius Damas amesema kuwa, Serikali inaingia garama kubwa sana katika
kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Amesema kuwa, Serikali
imeandaa mpango kazi wa kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto
kwa lengo la kupunguza vitendo hivyo kwa asilimia 50 kabla ya 2022.
"Tumejipanga
kuweka madawati ya kijinsia shule zote ili wanafunzi waweze kutoa taarifa za
vitendo vya ukatili wanapofanyiwa ikiwemo shuleni, majumbani na sehem
nyengine"amesema Damas.
Comments