VIONGOZI WA DINI WAWATAKA WATANZANIA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI
VIONGOZI WA DINI WAWATAKA WATANZANIA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI
Naye mjumbe wa baraza la ulamaa [Bakwata Taifa]Sheikh Issa Mohammed Issa amesema kuwa kongamano hilo la viongozi wa dini mbali mbali linapaswa kuja na mapendekezo yatakalolijenga taifa letu kwa umoja na amani kwani viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuendeleza amani kupitia mafundisho yao katika nyumba za ibada.
Kwa upande wake mkuu wa polisi Mkoa wa Temeke, Amon Kakwale akizungumza kwa niaba ya IGP Simon Sirro katika mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini kujadili amani na maendeleo baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.amesema viongozi wa dini wanafanya kazi kubwa ya kuhubiri amani jambo linalowarahisishia kazi polisi katika utekelezaji wa majukumu yao.
“Sisi ni makamanda wa kimwili na kiakili, kazi yetu ni kuwakamata na kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria wanaovunja amani kwa namna yeyote ile. Ninyi wenzetu ni makamanda wa kiroho, mnafanya doria za kiroho kusaidia kuwafanya watu kuwa na hofu ya Mungu na kutambua umuhimu wa kulinda na kuitunza amani,” amesema Kakwale.
Kamanda huyo ameongeza kuwa ipo migogoro mingi ambayo viongozi wa dini wanatumia nyumba za Ibada kuitatua kwa lengo la kunusuru nchi kuingia kwenye machafuko.
Kwa upande wake, Askofu Jacob Chimeledya amesema ipo haja kwa viongozi wa dini kukutana na wa vyama vya siasa kujadili mustakabali wa amani ya Taifa hili.
Comments