WAZIRI DKT NCHEMBA AAGIZA MAFUNZO YA SHERIA KUANZA KUTOLEWA KWA LUGHA YA KISWAHILI [LAW SCHOOL OF TANZANIA]

 

WAZIRI DKT NCHEMBA  AAGIZA  MAFUNZO YA  SHERIA KUANZA KUTOLEWA KWA LUGHA YA KISWAHILI [LAW SCHOOL OF TANZANIA]





Dar es salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Mwigulu Nchemba ameiagiza Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo [LST] kuhakikisha mafunzo wanayatoa kwa wanafunzi yawe na tija kwa wananchi kwa kutumia lugha ya kiswahili kwani wanaenda kuwahudumia watu ambaao wengi wao  hawafahamu Lugha ya kingereza .

Agizo hilo amelitoa leo Jijini Dar es salaam kwa katibu mkuu wa wizara hiyo katika ziara yake fupi alipotembelea taasisi hiyo   ambayo imekuwa ni sehemu muhimu ya kuwapika mawakili na wanasheria kwa vitendo kwenda kuwahudumia wananchi kwa lugha ya kiswahili wanayoielewa na mashauri wanayoenda kuwaandikia wawaandikie kwa lugha wanayoielewa kwani wengine wameshindwa kutambua haki zao kutokana na lugha ya kingereza wanayoandikiwa hivyo amemtaka katibu mkuu kuangalia jinsi sheria itakavyotafsiriwa kwa lugha ya kiswahili na kutumiwa na taasisi hiyo ya mafunzo kwa vitendo.

Sanjari na hayo alisema baadhi ya wananchi wamejikuta sintofahamu kukosa wa kuwafasiria lugha ya kingereza kutokana na mazingira wanauoishi hali hiyo ya kutumia kingereza ni kuwatesa wananchi na kuonekana bado tupo na ukoloni mamboleo wa lugha.

'Wananchi wanaumia sana wanapofika mahakamani mashauri wanaapoandikiwa kwa lugha ya kingereza hujikuta wakitumia muda mrefu kutafuta wa kuwafasiria kwa lugha wanayoielewa hali inayosababisha baadhi yao hadi kuelewa mida unakuwa umeenda na kuchelewa kukata rufaa,alisema Dkt Nchemba

Hata hivyo aliagiza Wizara na Taasisi  kuwatafuta wataalamu watakaofasiri sheria zote kwenda kwa lugha ya kiswahili ili kuepuka aibu ya baadae kutafuta wataalamu kutoka nje ya Nchi kufasiri sheria kuja katika Lugha yetu mama(kiswahi) ambapo ni aibu.

"Lazima ifike mahali mahali wananchi wetu wapumue na lugha hii ya kingereza inashangaza mahakamani tunawahoji kwa kiswahili cha ajabu tunawaandikia mashauri kwa kingereza"alisema Dkt Nchemba

Nae Naibu Waziri wa Katiba na sheria Geophrey Pinda alisema wanasheria wanahitajika kila mahali kuanzia mijini na vijijini na hivyo chuo hicho kwaandae vizuri kuwatumikia wananchi wao.

Ameongeza kuwa Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania ni sehemu ya ukombozi kwa wananchi hivyo kuna kila sababu ya kutengeneza chombo kama hicho kuwafikia wananchi kirahisi.




 
 



Waziri wa katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba akisisitiza jambo wakati akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) 

Waziri wa katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba akisisitiza jambo wakati akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) 
Waziri wa katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba akikagua maabara ya Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) 
Naibu Waziri wa katiba na Sheria Mhe Geofrey Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) 
Waziri wa katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba akisisitiza jambo wakati akizungumza na Menejimenti ya Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) 

Mkuu wa Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (Law School of Tanzania) Jaji Dkt. Benhajj Masoud wakati akiwa katika siku ya pili ya ziara ya kikazi Jijini Dar es salaam tarehe 22 Disemba 2020.


PICHA NA MATIUS CANAL.


Comments