Skip to main content

DCEA YAWASHIKILIA WATU WATATU KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA

 

DCEA YAWASHIKILIA WATATU,TUHUMA ZA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA

 





Na Mwandishi wetu


Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya (DCEA)  inawashikilia watuhumiwa watatu kwa tuhuma za kujihusisha na biashara za dawa za kulevya aina ya heroin.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kamishna Jenerali wa DCEA, James Kaji, amesema watu hao ni Anadhati Rashid Mchongeza umri miaka 20, Emanuel Msakuzi umri miaka 23, pamoja na Kulwa Pazi Shamas umri miaka 49 maaruf mama udodi.


Amesema kuwa, Januari, 22 mwaka huu katika eneo la kunduchi pwani kauzeni jijini Dar es Salaam watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na unga unaodhaniwa kua ni dawa za kulevya aina ya Heroin kiasi cha gram 400 na majani makavu ya bangi puli moja kiasi hicho ni sawa kete 30 za bangi.


Ameongeza kuwa, mamlaka baada ya kufanya upekuzi walifanikiwa kukamata kiasi hicho cha dawa zikiwa zimehifadhiwa ndani ya mfuko wa nailon, hivyo  inaendelea kuwashikilia watuhumiwa hao na watafikishwa mahakani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.


Katika hatua nyengine, mamlaka katika kipindi cha mwezi Nov 2020, illifanikiwa kushinda kesi kwa Mahakama kumtia hatiani mfanyabiashara maaruf jijini Tanga, Yanga Omar Yanga maaruf Raisi wa Tanga kwa kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya aina Heroin uzito wa gram 1052.63.


Hata hivyo, mamlaka imefanikiwa kufungua vituo vingine vitatu vya kutolea tiba ya methadone ikiwemo Tanga, Bagamoyo pamoja na hospital ya Tumbi Pwani sambamba na vituo hivyo vipya lakini pia imeongeza wigo wa upatikanaji wa tiba ya uraibu wa dawa za kulevya.


"Mamlaka inaendelea kutoa elimu juu ya tatizo la dawa za kulevya kwa njia mbalimbali ikiwemo Matukio makubwa ya kitaifa na vyombo vya habari, kutoa mafunzo  kwa wadau mbalimbali zaidi ya 500 wakiwemo madereva wa malori, wajasiriamali wanaotumia kemikali,pamoja na maafisa biashara "amesema Kamishna Jeneral James.

Comments