[NEEC]YAWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA KATIKA MAONYESHO YA 4 YA MIFUKO NA PROGRAME ZA UWEZESHAJI
[NEEC] YAWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA KATIKA MAONYESHO YA 4 YA MIFUKO NA PROGRAME ZA UWEZESHAJI.
DAR ES SALAAM.
Wananchi wa
jiji la Arusha na mikoa ya jirani wametakiwa kujitokeza kwa wingi na
kuchangamkia fursa katika maonyesho ya nne ya mifuko na program za uwezeshaji wananchi kiuchumi
yatakayofanyika jijini humo mwezi february 2021.
Akitoa
taarifa mbele ya wabahabari jijini Dar es salaam katibu mtendaji wa baraza la
Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi
[NEEC] Bi Beng'i Issa amesema kuwa
maonyesho hayo yana dhumuni la kukuza uelewa kwa wananchi kuhusu uwepo,majukumu
na vigezo vinavyotumiwa katika kutoa huduma za mifuko ya uwezeshaji ili
kuhamasisha wananchi kunufaika na fursa zilizopo katika mifuko hiyo pamoja na
kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujenga utamaduni wa kuweka akiba.
Aidha katibu
huyo mtendaji wa [NEEC] ameongeza kuwa watanzania wanapaswa kuwa na utaratibu
mzuri wa kuweka akiba na kuwekeza katika miradi yenye kuleta faida kupitia
uanzishwaji na uimarishwaji wa vikundi vya kifedha vya kijamii ikiwemo Vikoba.
Hata hivyo
ameendelea kuwa katika maonyesho hayo taasisi za umma,binafsi ,vikundi vya
kifedha,mashirika ya kimataifa na asasi za kiraia zitashiriki kikamilifu
maonyesho hayo yaliyoandaliwa na baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi [NEEC] ambapo
yatahusisha mikoa yote ya kanda ya kaskazini ikiwemo,Kilimanjaro,Tanga,Manyara
na Arusha.
Maonyesho
hayo yatafanyika katika viwanja vya sheikh
Amri Abeid [Stadim] katika jiji la
Arusha kuanzia february 7 hadi 13 mwaka huu ambapo mgeni rasmi katika
maonyesho hayo anatarajiwa kuwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
MH. KASIM MAJALIWA
Comments