WAZIRI KALEMANI AKUTANA NA WADAU WA GESI NA VIFAA VYA USAMBAZAJI WA NISHATI ,ASEMA USAMBAZAJI WA NISHATI HIYO MAJUMBANIN UMEONGEZEKA





Dar es salaam.


Katika kuhakikisha watanzania wananufaika na matumizi ya nishati na gesi Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema Mradi wa usambazaji wa Nishati ya Gesi majumbani umeongezeka kutoka Kaya 70 hadi kufikia Kaya 1000 kwa Miaka mitatu.

Dkt. Kalemani Ameyasema Hayo  jijini Dar Es Salaam Katika Mkutano Ulio wakutanisha Wadau wa kampuni zinazojishughulisha na biashara ya usambazaji wa NISHATI na Vifaa vya Nishati ulioandaliwa na Shirika la maendeleo ya Petroli Nchini TPDC.

Waziri Kalemani amesema kuwa Tayari Serikali imetenga Sh. Trilioni 1 kueleka Gesi Majumbani na kuunganisha Nishati hiyo kwenye Magari Pamoja na Trilion 4 kupeleka Nishati ya Gesi kwenye viwanda Nchini.

Hata hivyo, ametoa wito kwa Wadau wa viwanda kwa kutengeneza Vifaa vya kusafirisha Nishati ya mafuta na gesi kuanza kuzalisha Vifaa hivyo, ili kuondokana na Gharama za kununua Vifaa hivyo Nje ya Nchi kwani husababisha kuchelewesha Miradi hiyo.

Awali akizungumza kwenye Mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la maendeleo la Petroli TPDC Dkt. James Mataragio amesema wanaendelea na ujenzi wa vituo vitano vya kujaza gesi alisia kwenye magari katika mkoa wa dar es salaam huku kukiwa na mpango wa kupeleka nishati hiyo jijini dodoma

Comments