WAZIRI SIMBACHAWENE ATEMBELEA KIKOSI CHA WANAMAJI, BANDARI JIJINI DAR ES SALAAM
WAZIRI SIMBACHAWENE ATEMBELEA KIKOSI CHA WANAMAJI, BANDARI JIJINI DAR ES SALAAM
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akimpongeza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, baada ya kukabidhiwa gari aina ya Toyota GX V8 (inayoonekana) iliyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli kwa Ofisi ya Kanda Maalum. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (wapili kulia), akimwangalia Askari Mbwa wa Kituo cha Polisi Bandari, jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara katika Kikosi hicho, leo. Simbachawene ametoa siku saba kwa Jeshi la Polisi kuwepo kwa Bajeti ya Chakula cha Mbwa Askari waliopo wawili wa Kituo cha Polisi Bandari ipatakane ili Mbwa hao waweze kupatiwa chakula cha kutosha na kuwawezesha kufanya kazi za ulinzi katika Bandari hiyo. Watatu kulia ni Msimamizi wa Askari Mbwa hao, Richard Mshuza, akitoa maelezo ya kazi anazofanya Mbwa huyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati mstari wa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na Makamanda na Maafisa mbalimbali wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ofisi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa (wapili kushoto-mstari wa mbele), jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (watatu kulia), akiziangalia Boti za Polisi (hazipo pichani) kabla ya kuzipanda na kuzunguka nazo Bahari ya Hindi, kuona jinsi zinavyofanya kazi za kusaka wahalifu Baharini. Wapili kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Polisi Wanamaji Nchini, ACP Evance Mwijage akimuonyesha Waziri huyo kazi mbalimbali zinazofanywa na Boti hizo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Makamanda na Maafisa mbalimbali wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ofisi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa (watatu kulia). Simbachawene amewataka viongozi hao kufuata maadili ya Jeshi kwa kuwa waadilifu pamoja na kuwahudumia wananchi kwa haki. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akimpa maelekezo Mkuu wa Kituo cha Polisi Bandari, ASP Jeronimo Simon (katikati), wakati Waziri huyo alipofanya ziara katika Kituo hicho, jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Comments