WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO {MACHINGA]WA KARIAKOO,WAIPONGEZA SERIKALI KUIFANYA TAMISEMI KUWA 'MLEZI' WAO ,WAIOMBA SERIKALI KUWAWEKEA MFUMO WA KUWA NA VIONGOZI WA KUCHAGULIWA.
WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO {MACHINGA]WA KARIAKOO,WAIPONGEZA SERIKALI KUIFANYA TAMISEMI KUWA MLEZI WAO ,WAIOMBA SERIKALI KUWAWEKEA MFUMO WA KUWA NA VIONGOZI WA KUCHAGULIWA.
Dar es salaam.
Wafanyabiashara ndogondogo wanaofanya biashara eneo la karikakoo Jijini Dar es salaam maarufu kama WAMACHINGA wameiomba Serikali kuwawekea wafanyabiashara hao mfumo madhubuti wa kuwa na uongozi wa kuchaguliwa kwa kura na wamachinga wenyewe ili kuweza kuwatatulia kero zao kwa urahisi.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya kuwepo kwa malalamiko juu ya uongozi uliopo ambao umedaiwa kukaa zaidi ya miaka 7 bila ya kuchaguliwa na wamachinga wenyewe.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam jana msemaji wa muda wa wamachinga wa karikoo Masud Issa Chauka alisema uongozi uliopo kwa sasa ni batili kutokana na kutokuwa rasmi katika utendaji wa kazi.
Alisema mfumo uliopo kwa sasa sio rafiki kwa wamachinga hivyo upo umuhimu kwa kuwa na viongozi halali waliochaguliwa kwa mujibu wa katiba ya Chama cha wamachinga kariakoo(TAWASO) ambao unaozingatia katiba ya Chama hicho.
" Wamachinga wote wanaofanya biashara ndogo ndogo nchi nzima wanapaswa kutegeneza mfumo wa kuwa wa viongozi wa kuchaguliwa na kupigiwa kura na kuwa na ukomo wa muda wa kishikilia nyadhifa "alisema Chauka
Chauka alisisitiza kuwa lengo la kuwa na viongozi waliochaguliwa na wamachinga wenyewe ni kuimarisha utendaji kazi wa sekta ikue kwa kasi na kukuza uchumi ambao utasaidia kuongeza pato la taifa .
Pia alisema wamachinga wanaiunga mkono Shirikisho la Umoja wa vyama vya Wamachinga Taifa ( SHIUMA) lakini wanaitaji kufanyika kwa marekebisho kwa kuchangua viongozi kuanzia ngazi za wilaya,Mkoa na Taifa pamoja na kuunda shirikisho kwa makubaliano ya pande zote.
"Tunaiomba serikali ituangalie sisi wamachinga kuanzia mfumo wa chini kwani tunakabiliwa na chagamoto nyingi zinazoitajika kutatuliwa ..
Uwepo wa viongozi waliochaguliwa na wamachinga utatusaidia kutatua kero zinazotukabili kwa muda mrefu.
Hata hivyo aliipogeza serikali kupitia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kwa kuitisha mkutano na wamachinga wote Tanzania uliofanyika hivi karibuni ambao ulilenga kijadili chagamoto mbalimbali zinazowakabili.
Hata hivyo katika hatua nyingine wamachinga hao wameipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli kwa kuitambua na kuithamini sekta ya wamachinga na hatimaye kuwawekea mfumo mzuri wa kiutendaji usio na bugdha sambamba na kuwapatia wizara ya TAMISEMI kama wizara mama ya kuwasimamia wafanyabiashara ndogondogo hao.
Kwa upande wake mmoja wa waasisi wa Chama cha wafamachinga karikaoo KAWASO, Rajabu Mahundu alisema mpaka sasa imepita takribani miaka 7 bila ya kuwa na uongozi halali waliochaguliwa kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho
Mahundu aliliiomba serikali kupitia Wizara ya nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kuwasaidia kuhamasisha viongozi wa ngazi za juu kuwafata wamachinga ngazi za nchini kusikiliza kero zao.
" Kikao kazi kilichofanyika hivi karibuni na waziri mkuu Kassim Majaliwa kitakwenda kuzitafutia ufumbuzi kwa kuweza kutusaidia kutukutanisha na sekta za kifedha"alisema Mahundu.
Katika hatua nyingine aliwaomba wakurungezi na wakuu wa wilaya wote wa Halmashauri kuwaimiza wamachinga kwenye maeneo yao kwenda kuchukia vitambulisho vipya kwa ajili ya kuendelea na kazi zao ili kuchangia pato kwa taifa.
Comments