MIRADI 51 YASAJILIWA NA KITUO CHA UWEKEZAJI NCHINI TIC KATIKA KIPINDI CHA JANUARY/MACHI 2021,MAZINGIRA YA UWEKEZAJI YABORESHWA







Katika kuendelea kuonyesha kuwa sekta ya uwekezaji imekuwa kwa kasi Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC)kimesema katika kipindi cha mwezi januari hadi machi mwaka huu,kimefanikiwa kusajili jumla ya miradi mipya 51 yenye thamani ya dola za kimarekani 451 milioni huku kikibainisha sekta ya viwada kuongoza katika miradi hiyo kwa kuwa na miradi 30 sawa na asilimia 59 ya miradi yote.

Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho daktari Maduhu Kazi wakati wa utoaji wa taarifa ya robo tatu mwaka 2020/2021 kwa waandishi wa habari.

Daktari Kazi amesema miradi hiyo inatarajia kuzalisha ajira mpya 4,272 sawa na ongezeko la asilimia 3.5 ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka jana ambapo miradi 54 ilisajiliwa ambyo ilitarajiwa kuwekeza mtaji wa dola za kimarekani 283 milioni iliyozalisha ajira 4,127

"sekta iliyoongoza kwa uzalishaji wa ajira mpya ni utalii ambapo inategemea kuzalisha ajira 572 sawa na asilimia 13.4 ya ajira zote,"amesema dkt Kazi.

Amebainisha kuwa kati ya miradi 51 iliyosajiliwa mwaka huu miradi 13 sawa na asilimia 25 ni miradi ya wawekezaji wa ndani,miradi 26 sawa na asilimia 51 ni miradi ya wawekezaji wa kigeni,na kusisitiza miradi 12 sawa na asilimia 24 ni miradi ya ubia kati ya watanzania na wageni.

Aidha amesema TIC kinatunza kumbukumbu za miradi ya uwekezaji iliyosajiliwa hivyo wawekezaji ambao wamewekeza nchini bila kupitia kituo hicho hawako katika takwimu hizo  badala yake wawekezaji wengine husajiliwa na EPZA,Tume ya madini na wengne huwekeza bila kupitia katika taasisi hizo.

Ameongeza kuwa katika kuendelea kuboresha uwekezaji nchini kituo hicho kimejiwekea mikakati mbalimbali ikiwemo kuendelea kuboresha mfumo wa kusajili miradi unaotumiwa na kituo hicho,kuunganisha mfumo wa kusajili miradi (TIW)unaotumika na TIC na mifumo mingine inayohudumia wawekezaji nchini.

Mikakati mingine ni kuhamasisha zaidi uwekezaji kwa wazawa na ubia,kufuatilia kwa karibu wawekezaji kwa lengo la kung'amua changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi yao,pamoja na kuboresha zaidi matumizi ya tehama katika shughuli zote za kunadi na kuhumia wawekezaji.

Aidha ameongeza kuwa kituo hicho  miongoni mwa miradi iliyosajiliwa mwezi Aprili mwaka jana ni Mradi wa Kiwanda Kikubwa cha Mbolea cha Kampuni ya Itracom Fertilizers unaojengwa Dodoma utakaowekeza dola za Kimarekani milioni 180 na kuzalisha ajira za moja kwa moja milioni 3000 ambapo tani za mbolea 500,000.

Dkt.  Kazi alisema kituo hicho kinaendelea kuwakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini kwani mazingira ya uwekezaji yameboreshwa zaidi Kuhusu miradi iliyosajiliwa katika kipindi cha mwezi julai 2020 hadi mwezi march 2021 kituo hicho kimesema jumla ya miradi 151 imesajiliwa ambapo inatarajia kuwekeza mtaji wa dola za kimarekanini milioni 987.04 na kutoa ajira 13,857 huku sekta ya viwanda ikiendelea kuongoza katika miradi iliyosajiliwa na kituo cha uwekezaji Tanzania ambapo jumla ya miradi 94 sawa na asilimia 62.25 yenye mtaji wa jumla ya dola za kimarekani milioni 463.17 ambayo inatarajiwa kutoa ajira kwa watanzania wapatao 9,220

Comments