Ten/Met yakutanisha wadau wa elimu Afrika kujadili mustakabali wa elimu hapa nchini.




Dar es salaam.

Wadau wa elimu hapa nchini wametakiwa kushirikiana vyema na serikali katika kuhakikisha mazingira na kiwango cha elimu kinachotolewa hapa nchini kinaendana na mabadiliko ya sekta hiyo kidunia kwa kuuondoa mfumo wa utoaji hafifu wa elimu unaoyakumba mataifa yanayoendelea ikiwemo Tanzania.

 Hayo yamesememwa na Rais mstaafu wa awamu ya nne wa serikali ya Jamhuri ya Tanzania,Dkt  Jakaya Kikwete wakati akifungua kongamano la  kimataifa la elimu bora lililoandaliwa na mtandao wa elimu Tanzania [TenMet]unaofanyika jijini Dar es salaam unaojadili masuala mbali mbali ya elimu ikiwemo Mchango wa serikali katika kuimarisha elimu nyakati za maafa ikiwemo magonjwa ya mlipuko mfano COVID-19, Hatima ya elimu ya juu: Kwanini watahiniwa wengi hawaajiriki na masuala mengine ya elimu lengo ikiwa ni kuhakikisha kunakuwepo na maboresho na maendeleo yanaochagizwa na wadau wa sekta hiyo.


 Dkt Kikwete amesema changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya elimu hapa nchini ikiwemo  utoaji hafifu wa elimu unaotolewa nchini Tanzania kuna hatari ya kutoweka kwa nusu ya ajira zilizopo ifikapo mwaka 2050 kutokana na wanaopewa elimu hizo kutokidhi vigezo vya kuajirika.


Hata hivyo ameendelea , kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na tume ya kimataifa ya elimu ambayo yeye ni mjumbe, unaonyesha kuwa  elimu inayotolewa barani Afrika  kwa sasa ilitolewa miaka 50 hadi 70 iliyopita kwa nchi zilizoendelea jambo linalokwamisha nchi nyingi za kiafrika kutozalisha wasomi wanaoendana na soko la ajira la kimataifa.


"Sisi bado tunatumia chaki, wakati wenzetu wanatumia tablets, tuliona kuwa kuna watu zaidi ya milioni 263 waliotakiwa kuwa shule lakini hawapo, kati yao milioni 100 wapo Afrika,  waliopo shule wengi hawamalizi wanaishia njiani, asilimia 67 ndio wamemaliza,hii ni sawa na asilimia 33 ni idadi kubwa," amesema Rais Kikwete.


    Kuhusu suala la teknololjia amesema kuwa  kuwa, katika kufikia matumizi ya teknolojia, ni vyema kuwepo na uwekezaji mkubwa katika elimu ili vijana wa Afrika wasiwe watazamaji katika masuala ya ukuaji wa uchumi wanatakiwa kushiriki ipasavyo.


Hata hivyo, amesema ili kuendana na kasi ya matumizi ya sayansi na Teknolojia  kila shule inatakiwa kuunganishwa  internate katika ufundishaji ili kuepukana na athari ambazo zinaweza kuepukika.


"Tumeona wakati wa corona, moja hatua zilizochukuliwa ni kufunga shule, wanafunzi wetu hawakusoma, walicheza rede, lakini nchi zilizoendelea shule zilifungwa na watoto wakaendelea kusoma."amesema Rais Kikwete.


Amesema kuwa,wakati  alipokua Rais walianzisha matumizi ya intaneti katika ufundishaji, ambapo waliwekeza sana kwenye mkongo wa Taifa, lengo lilikuwa ni kuhakikisha kila shule, hospitali ziunganishwe na intaneti ili mwalimu mmoja aweze kufundisha nchi nzima kwa kutumia Teknolojia.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tenmet, Dk John Kalage ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki Elimu amesema kongamano hilo litajadili kwa kina namna bora ya kuekeza katika masuala ya Teknolojia ya kuweza elimu bora nchini.


Amesema kuwa, katika kongamano hilo pia kutakuwepo na mada kadhaa ambazo zitajadiliwa kwa kina ikiwemo ni namna gani Serikali imejipanga ikitokea changamoto nyengine zinazohusu elimu zitaweza kutatulika kwa haraka bila kuleta athari.


Kwa upande wake, Mratibu wa Kitaifa mtandao wa elimu Tanzania (TenMet)  Ochola Wayoga amesema kuwa, asasi za kiraia zina mchango mkubwa sana katika kuisaidia Serikali katika kuboresha elimu ya Tanzania.


Aidha amesema kuwa, mkutano huo umewakutanisha washiriki kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Uganda, Kenya, Malawi, Lushoto na Zanmbia lemgo ikiwa ni kujadili kwa upana namna ya kuboresha elimu kwa Afrika na kuwawezesha vijana kuweza kutumia Teknolojia.


Hata hivyo, Bw. Wayoga aliongeza kuwa mkutano huo utaendeshwa katika mfumo wa mijadala, ambapo mada mbalimbali zinazohusiana na elimu zitajadiliwa ili kutoa fursa kwa wadau kujadiliana zaidi. Na kutakuwa na uwasilishaji wa tafiti za kielimu wenye lengo la kuufahamisha umma hali na mwenendo wa elimu ya Tanzania kuanzia ngazi ya elimu ya awali, elimu ya msingi, sekondari hadi chuo kikuu. 


Mkutano huo ulioanza may 18 mwaka huu unatarajiwa kumalizika may 20,2021 na utakuja na maazimio mbalimbali kuhusu mustakabali wa elimu ya Taanzania na Afrika kwa ujumla.



Comments