Skip to main content

DMK GLOBAL YAJA NA SHOW YA DAVIDO

 

DMK GLOBAL KUANDAA SHOW BABUKUBWA YA DAVIDO



Na Mwandishi wetu

Promota maarufu nchini Tanzania DMK Global ambae amekua akiandaa show mbalimbali za wasanii kimataifa anatarajia kufanya show kubwa ya Davido nchini Nigeria.

Show hiyo kubwa itakayofanyika nchini Nigeria June 18, mwaka huu ambayo itajulikana kama Davido unity Concert itakayofanyika bila mashabiki ambapo watu wataona show hiyo kupitia www.SHRUTV.Com/Concert ambapo watu watatakiwa kulipia dola tano za kimarekani sawa na sh 10,000 pesa za kitanzania.

Amesema kuwa,show hiyo itafanyika saa nne usiku ambapo mashabiki hata walioko nchini Nigeria hawatoingia uwanjani ambapo fedha zitakazopatikana zitakwenda kuwasaidia watoto Yatima nchini Tanzania na nje ya Tanzania.



"Sababu ya kufanya show bila mashabiki ni kutokana na ugonjwa wa Covide 19 ambapo nchi nyingi bado hazijawa sawa,lakini duniani kote wakiwa sawa basi zitafanyika show kama mwanzo mashabiki wataingia uwanjani"amesema DMK Global

Comments