Skip to main content

KUFUATIA KUACHIWA HURU MASHEIKH JUMUIYA YA UAMSHO,TAASISI YA HIZB UT TAHRIR YAOMBA MAHABUSU WENGINE KUACHIWA HURU

 

KUFUATIA KUACHIWA HURU MASHEIKH JUMUIYA YA UAMSHO,TAASISI YA HIZB UT TAHRIR YAOMBA MAHABUSU WENGINE KUACHIWA HURU

 


Na Mwandishi wetu


Taasisi ya Hizb Ut Tahrir imeiomba Serikali kupitia Mkurugenzi wa Mashtaka Dpp kuwafutia kesi watuhumiwa wengine wa makosa ya ugaidi ambao wapo mahabusu kwa miaka minne sasa katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam,Arusha,Tanga pamoja na mkoa wa Mtwara.


Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kumtaka DPP kuwafutia kesi watuhumiwa wote ambao hawana hatia, ambapo June 16 mwaka huu watuhumiwa 36 wa makosa ya kigaidi waliachiwa huru.


Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dar es Salaam, Muwakilishi kwa vyombo vya habari wa Taasisi ya Hizb Ut Tahriri, Masoud Msellem amesema kuwa,kufutwa Mashtaka ya Uamsho ni hatua muhimu ya kutoa moyo, lakini huo uwe mwanzo kwa Taasisi za kusimamia haki kwani kuna mahabusu wengi wa Mashtaka ya aina hiyo.


Aidha, amesema sheria ya makosa ya ugaidi imekua imelalamikiwa tangu kuanzishwa kwake kutokana na kuwabana watuhumiwa kwa kuwanyima haki za msingi ikiwemo dhamana pamoja na fidia baada ya kuwaweka mahabusu kwa miaka mingi.


"Tunavitaka vyombo vya kisheria kusimamamia haki vijizatiti katika majukumu yao kwa weledi, uaminifu na haki kama alivyosema Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Sylvester Mwakitabu karibuni katika vyombo vya habari"amesema Msellem.


Amesema kuwa, mahabusu wote hao wanateseka katika mazingira duni kwa miaka mingi kwa mgongo wa sheria ya ugaidi ambayo Ina mamlaka ambayo inambana mtuhumiwa na kupelekea kesi zao kutosikilizwa kwa wakati na kutolewa hukumu kwa madai kuwa upelelezi haujakamilika.


Hata hivyo, ameipongeza  Serikali ya awamu ya sita ya Samia Suluhu Hassan kwa hatua walizozichukua kuwaachia watuhumiwa hao wa makosa ya ugaidi, huku akielezea  uislamu sio dini ya ugaidi na wala haijawahi kuwa hivyo.

Comments