Skip to main content

MUFTI MKUU WA TANZANIA AOMBA UPELELEZI WA MASHEKHE WA UAMSHO UHARAKISHWE

 

MUFTI MKUU WA TANZANIA AOMBA UPELELEZI WA MASHEKHE WA UAMSHO UHARAKISHWE


Na Mwandishi wetu


Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar bin Zuber ameiomba Serikali kupitia Mahakama kuharakisha upelelezi wa mashekhe wa Uamsho kwani wamekaa gerezani kwa muda mrefu bila kutolewa hukumu yoyote.


Wito huo ameutoa leo jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari walipokutana na viongozi wa dini mbalimbali kwa ajili ya kuzungumza mambo mbalimbali yenye mahusiano ya kujenga udugu na ujamaa.


"Suala la watu waliowekwa ndani hasa waislam ni suala linaloonyesha wamekaa muda mrefu kama miaka 9 au 10, naiomba Mamlaka husika, Mahakama, DPP na Mamlaka nyingine pamoja na Serikali kwa ujumla kesi zao ziharakishwe watakaoonekana wana matatizo basi sheria ichukue mkondo wake"amesema Mufti Abubakar


Amesema kuwa, kesi ya mashekhe hao imechukua muda mrefu sana na kuleta taharuki hivyo, ni vyema watakao onekana hawana matatizo basi waachiliwe ili kulinda amani na upendo uliopo ndani ya Taifa la Tanzania


Kwa upande wake, Askofu Nelso Kisare Kanisa la Mennonite Tanzania amesema kuwa, wanapozungumzia ukuaji wa Uchumi watanzania wote wanahitaji kuwa na Uchumi mzuri ili kila mtu aweze kuiona nchi hii kuwa ni nchi nzuri na kila mtu anaweza akapata chakula chake cha kila siku.


"Tunapozungumzia suala la amani sisi sote tunatamani kuwa na amani kama watanzania na hili halimuhusu mtu kama dini yake, sisi sote watanzania tunahitaji kuimarisha amani

 maji safi na salama hayo hayahusiani tena na dini lakini yanatukusanya kwa pamoja"am Askofu Askofu Kisare.


Naye, Askofu Peter Konki Askofu mkuu wa elim Pentekosti na Mwenyekiti wa CPCT amesema kuwa viongozi wa dini  S kama wanapaswa kusapoti na kuvichochea vitu vyetu  ili Taifa letu liendelee kuwa zuri, salama na mahali ambapo kilamtu atafurahia kui

Comments