WADAU HAKI ZA BINADAMU,WATOTO WAZUNGUMZA KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA.
WADAU HAKI ZA BINADAMU,WATOTO WAZUNGUMZA KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA.
Na Mwandishi wetu ,Dae es salaam
Juni 16 kila mwaka bara la Afrika huadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika tangu kuidhinishwa kwa siku hiyo na Umoja wa Afrika mwaka 1991. Umoja wa Afrika ulianzisha Siku ya Mtoto wa Afrika kama sehemu ya kuwakumbuka na kutambua mchango wa watoto waliopoteza maisha katika mauaji yaliyotokea huko Soweto, Afrika ya Kusini wakati watoto walipoandamana kudai haki zao za msingi.
Katika nchi mbali ikiwemo Tanzania maadhimisho hayo hufanyika pia katika maeneo mbali mbali hapa nchini hali iliyopelea wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia ikiwemo haki za watoto kujitokeza na kuiomba jamii kuacha tabia ya kuficha watoto wenye ulemavu kwani wanahaki sawa na wengine.
Kunako Mwaka 1991, Wakuu wa Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika, OAU walianzisha Siku ya Mtoto wa Afrika kama kumbukumbu ya uasi dhidi ya wanafunzi uliotokea hapo tarehe 16 Juni 1976 huko Soweto, Afrika Kusini. Wakati huo, wanafunzi watoto wadogo waliandamana, mosi kupinga mfumo na elimu duni waliokuwa wanapatiwa. Pili, waliitaka Serikali ya kibaguzi ya Afrika ya Kusini kuboresha mfumo wa lugha ya kufundishia. Siku ya Mtoto wa Afrika hutumika kuwakumbusha watoto wetu hatua ya kijasiri waliyoichukua wenzao huko Afrika Kusini katika kulinda utu, heshima na haki zao msingi. Watoto wanakumbushwa kwamba wanaweza kuleta mabadiliko hata wakiwa wadogo. Hii ni Siku ya Kimataifa inayopania kuboresha hali na mazingira ya elimu kwa watoto Barani Afrika.
Kwa hivyo, Hivyo Siku Ya Mtoto wa Afrika inaadhimishwa kwa kuangalia maslahi mapana ya watoto wa Afrika na inawapasa watu wazima kujitolea kwa hali na mali katika nafasi zao ili kushughulikia changamoto nyingi zinazokabili watoto katika Bara zima la Afrika. Watoto wanapaswa kulindwa dhidi ya ukatili na unyama wanaoweza kutendewa ndani na nje ya familia zao. Watoto wanapaswa kuepushwa ndoa na mimba za utotoni kwa kupewa na kurithishwa maadili mema. Kipindi cha janga la ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona, takwimu zinaonesha kwamba, kuna idadi kubwa ya watoto waliopata mimba kwa sababu ya kukaa muda mrefu majumbani mwao. Wazazi wanapaswa kuwajibika kikamilifu juu ya ulinzi na tunza ya watoto wao. Watoto wanapaswa kuepushwa na vishawishi kwa kuhakikisha kwamba, wanapata mahitaji yao msingi kwa wakati. Wafundwe pia kuwa na kiasi kwani katika maisha hawataweza kupata kila kitu wanachohitaji. Watoto wafundishwe umuhimu wa kuwa na nidhamu katika maisha! Waswahili wanasema, watoto wakilindwa vyema, watawaheshimu na kuwakumbuka wazazi wao!



Comments