Wamachinga Kariakoo Tuna Matumaini Makubwa na Rais SAMIA
Wamachinga Kariakoo Tuna Matumaini Makubwa na Rais SAMIA
Msemaji wa Wamachinga wa kariakoo Masoud Issah kifafanua jambo katoka mahojiano na mwandishi wa mtandao huu jijini Dar es salaam.
Wafanyabiashara wadogo (Wamachinga) wa soko la Kariakoo wamesema wanaimani na serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuhaidi kuendelea kumuunga mkono ili kuliletea Taifa maendeleo.
Wakitoa maono yao mara baada ya hotuba ya rais Samia Suluhu wakati akizungumza na wanawake jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine aliwasihi kujitambua na kufanya kazi kwa bidii huku akiwataka kuchangamkia fursa za masoko zilizopo.
Akizungumza kwa niaba ya wanawake hao msemaji wa Wamachinga wa kariakoo Masoud Issah alisema wamachinga wanawake wa kariakoo wamefurahishwa na kauli alizozitoa rais Samia nakwamba wanamuunga mkono ili kulifikisha taifa katika hatua kubwa zaidi ya maendeleo.
Alisema asilimia kubwa ya wajasiliamari hapa nchini ni wanawake ambapo wengi wao wanamiliki biashara ndogondogo lakini wapo pia wanao miliki viwanda vidogo na vikubwa hivyo wanahitaji msaada mkubwa katika kuwawezesha mikopo na kuwatengenezea mazingira mazuri ya masoko.
Alisema kwasasa wamachinga wa kariakoo wanapata mikopo kutoka taasisi za kifedha ambazo zimekuwa na masharti magumu ambayo yanawafanya wakina mama wengi kushindwa kurejesha mikopo hiyo ambapo wengi wanadidimia kibiashara.
Mfano unapochukua milioni moja benki unatakiwa kwanza ulipe elifu sabini na tano ofisi ya wamachinga,baada ya hapo ulipe elfu tano ya fomu halafu ndo uwe umekidhi vigezo vya kupata mkopo huo,na hata ukipata utasumbuliwa mno na watu wanaohitaji marejesho hali ambayo wamachinga wengi wanalalamika sana" alisema.
Alisema hizo fedha tunazolipa kabla yakuchukua mkopo hatujui wanazipeleka wapi, nakama zinaenda serikalini basi tunaomba serikali itusaidie kiondoa masharti haya kwani yanamdidimiza mfanyabiashara na sio kumuinua.
Alisema kumekuwepo mikopo ambayo ina ratibiwa na baadhi ya viongozi wa wamachinga kwa kufanya makubaliano na taasisi moja ya kifedha ili kuwakopesha wamachinga lakini hawajawahi kuitwa wamachinga wote kuelezwa namna mikopo itakavyotolewa na masharti yake ili wakubaliane kwa pamoja,ambapo amedai kuwa inawezekana uongozi uliopo upo kwa maslahi yake binafsi.
"Tunaomba sana serikali kupitia ofisi ya Mkurugenzi, mkuu wa wilaya na mkoa uje utusikilize wamachinga na wafanyabiashara hapa kariakoo, na tunapenda kuishauri serikali kuacha kusikiliza uongozi wa wamachinga moja kwa moja hawatapata ukweli wa mambo, tumefurahi kauli ya mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mhe. Amos Makalla kuwa anakuja kufumua mtandao wa kariakoo tuna muomba asichelewe aje tuondoe hizi kero." Alisema Issah
Alisema suala la wamachinga kupanga biashara zao kwenye barabara za mwendokasi na maeneo mengine yasiyostahili ni kutokana na uongozi mbovu wa wamachinga uliopo kwa sasa nakwamba wamachinga wa kariakoo niwasikivu endapo watelekezwa vizuri na kupangiwa sehemu za kufanyia biashara zao.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments