CHUO KIKUU CHA IRINGA (UoI) CHATAJA UPEKEE,UTOFAUTI WA KOZI ZAKE

CHUO KIKUU CHA IRINGA CHATAJA UPEKEE,UTOFAUTI WA KOZI ZAKE




Na Thadei Praygod

Dar es salaam.

 Katika kuhakikisha wanafunzi wa kitanzania wanapata elimu bora chuo kikuu cha Iringa kimewataka Wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini Tanzania  kuwa makini wanapochagua vyuo ili kupata vyuo vyenye ubora na umahiri wa kufundisha kwa vitendo zaidi.


Hayo yamesemwa  jijini na Dar es Salaam na Afisa Mahusiano na Masoko wa Chuo Kikuu Cha Iringa, Crispin Nyomoye alipokua katika maonyesho ya 16 ya vyuo vya elimu ya juu Sayansi na Teknolojia yanayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja ambapo amesema wanafunzi wengi wamekua wakichagua vyuo vya kufuata mikopo bila kuvipenda.

Amesema kuwa, kwa sasa Serikali imesema wanafunzi wote wataweza kupatiwa mikopo bila kuangalia shule aliotoka iwe ya Serikali ama binafsi hivyo ni muda wa kutafakari kwa kina kuchagua vyuo ambavyo vitaweza kuwapatia elimu bora na sio bora elimu.

Aidha,amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikitoa elimu kwa vitendo zaidi ya asilimia 90 ambapo utofauti wa chuo hicho na vyuo vyengine katika utoaji wa kozi hasa za sheria katika ngazi ya bachelor wanafunzi husoma miaka mitatu badala ya minne kama inavyofanya vvyuo vyengine.

Ameongeza kuwa, wanafunzi wanasoma katika chuo hicho wanakua na ujuzi na maarifa kutokana na elimu bora wanayopatiwa chuoni hapo, hivyo amewataka wazazi na walezi kuwapeleka vijana wao kusoma katika chuo hicho na kuchagua kozi mbalimbali.

Hata hivyo, amesema Chuo hicho kinatoa kozi katika ngazi mbalimbali ikiwemo cheti,diploma,degree na Masters katika kozi mbalimbali ikiwemo Sheria, Uandishi wa habari, Maendeleo ya jamii, Teknolojia ya habari (IT) pamoja na  Utalii.

Unaweza kuwasiliana na chuo hicho kupitia website yao ya www.uoi.ac.tz

Certificate Courses

  1. FACULTY OF THEOLOGY
    • Certificate in Divinity.
  2. FACULTY OF LAW
    • Certificate in Law.
  3. FACULTY OF PSYCHOLOGY
    • Certificate in Counselling Psychology.
  4. FACULTY OF BUSINESS AND ECONOMICS
    • Certificate in Business Administration.
    • Certificate in Business in Human Resources.
    • Certificate in Procurement and Supply Chain Management.
  5. FACULTY OF ARTS AND SOCIAL SCIENCES
    • Certificate in Journalism.
    • Certificate in Community Development.
  6. FACULTY OF SCIENCE AND EDUCATION
    • Certificate in Information Technology

Diploma Courses

  1. FACULTY OF THEOLOGY
    • Diploma in Divinity.
  2. FACULTY OF LAW
    • Diploma in Law.
  3. FACULTY OF PSYCHOLOGY
    • Diploma in Counselling Psychology.
  4. FACULTY OF BUSINESS AND ECONOMICS
    • Diploma in Business Administration.
    • Diploma in Business in Human Resource Management.
    • Diploma in Procurement and Supply Chain Management.
    • Diploma in Procurement and Material Management.
    • Diploma in Accountancy.
  5. FACULTY OF ARTS AND SOCIAL SCIENCES
    • Diploma in Journalism.
    • Diploma in Community Development.
    • Diploma in Leisure and tourism Studies.
  6. FACULTY OF SCIENCE AND EDUCATION
    • Diploma in Information Technology

Degree Courses

PROGRAMMES OFFERED FOR UNDERGRADUATE STUDIES

  1. FACULTY OF THEOLOGY
    • Bachelor of Divinity.
  2. FACULTY OF LAW        
    • Bachelor of Law.
  3. FACULTY OF PSYCHOLOGY
    • Bachelor of Counselling Psychology.
  4. FACULTY OF BUSINESS AND ECONOMICS
    • Bachelor of Business Administration (BBA).
    • Bachelor of Business in Marketing (BBM).
    • Bachelor of Business in Human Resources (BHR).
    • Bachelor of Procurement and Supply Chain Management (BBP).
    • Bachelor of Applied Marketing and Entrepreneurship (BAME).
    • Bachelor of Science in Accounting and Finance (BSc. AF).
    • Bachelor of Science in Economics and Finance (BEF).
  5. FACULTY OF ARTS AND SOCIAL SCIENCES
    • Bachelor of Arts in Community Development (BACD).
    • Bachelor of Arts in Journalism (BAJ).
    • Bachelor of Arts in Cultural Anthropology and Tourism (BACAT).
  6. FACULTY OF SCIENCE AND EDUCATION
    • Bachelor of Science in Information Technology (BSc. IT).
    • Bachelor of Education (Arts).
    • Bachelor of Education (Mathematics).

Comments